AKIBA BENKI YAZINDUA KAMPENI "TUPO MTAANI KWAKO"
Na Mwandishi wetu
ILI kuendana na kasi ya upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja, taasisi za kifedha zinatakiwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kwa kuwasogezea karibu ili kusaidia kupunguza adha ya kutumia muda mwingi kufuata huduma umbali mrefu na kuchelewa kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba Danford Muyango wakati akizindua rasmi kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo, Letsya Tower ambapo amesema watahakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi.
Aidha, amesema wapo mtaani kila mahali wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigital VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking ambapo uzinduzi huo utaendana sambamba na kupata wateja wengi zaidi.
Amesema kuwa, wamezindua rasmi program hiyo kupitia timu yao ya mauzo ambapo kwa sasa watafika popote, watazunguka nchi nzima ili kuhakikisha wateja wao wanapata huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo elimu ya mikopo, visa card, na kutumia huduma za kidigital
"Tumezindua rasmi program yetu ya TUPO MTAANI KWAKO kupitia timu yetu bobezi ya mauzo sasa tunakufika popote ulipo nchi nzima kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti , elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking" amesema Afisa biashara
Aidha, Muyango amesema pamoja na mambo mengine, pia program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ili kusambaza huduma hizo Kwa ukubwa zaidi.
Comments
Post a Comment