PAMBANO LA NOCK OUT YA MAMA KUPIGWA OCT 5, DAR

 




Na Mwandishi wetu,Dar 

Wadau na mashabiki wa boxing wajiandae kupokea burudani ya kutosha kutoka kwenye pambano la kimataifa la Knockout ya mama litakalopigwa katika viwanja vya magomeni sokoni jijini Dar es Salaam Ock 5 mwaka huu.

Pambano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Mafia Boxing Promotion ambapo pambano hilo litawakutanisha mabondia mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiweno Ibrahim Mafia kutoka Tanzania na Said Chino .



Akizungumzia kuhusu maandalizi ya pambano hilo mbele ya waandishi wa habari mapema leo Septemba 26,2024 Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Anthony Nurgazi amesema kwamba pambano hilo litawakutanisha mabondia Ibrahim Mafia Tz na Said Chino katika kuwania mkanada wa WBC.

"Kama ilivyo katika Mchezo wa mpira wa miguu,Rais Dkt Samia amekua akitoa zawadi ya fedha kwa kila Gori linalofungwa katika mechi za Kimataifa ili kuleta motisha kwa wachezaji,nasisi huku atujakaa mbali tumeamua kuja na pambano hili (Nockout ya Mama) mshindi atapata milioni kumi kama bonasi" amesema Nurgazi



Amesema kuwa pambano hilo la kimataifa litafanyika katika ukumbi wa City Centre Hall Magomeni, pamoja na mambo mengine, licha ya kutoa burudani limelenga kuwaenua mabondia watanzania kujulikana na kufanya kazi zenye kiwango ili waweze kufikia ndoto zao.

Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, Bondia Ibrahim Mafia Tz amesema kwamba amejiandaa vya kutosha na anaendelea kujiandaa vizuri ili aweze kukabiliana na mpinzani wake sambamba na kushinda pambano hilo.



"Mashabiki wa boxing musiwe na wasiwasi , nimejiandaa vya kutosha na naendelea kujiandaa kupigana na mpinzani wangu nitahakikisha mashabiki mutafurahia burudani hii wasiwe na wasiwsi ,nipo vizuri nawakaribisha wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia pambano siku hiyo" amesema.

Kwa upande wa bondia Said Chino amesema kuwa yupo tayari kupigana kwenye pambano hilo nakwamba kwa sasa anaendelea kujifua ili kuweza kumshinda mpinzani wake, ambapo ameahidi kushinda kwenye pambano hilo.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...