Posts

Showing posts from October, 2024

BUSHMAN SAFARI TRACKERS YATOA MSAADA WA PIKIPIKI 6 KWA ASKARI WA TAWA

Image
Na Joyce Ndunguru, Morogoro Katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika ulinzi wa rasilimali za wanyamapori nchini, Kampuni ya Bushman Safari Trackers iliyopo Mkoani Morogoro imetoa msaada wa pikipiki sita (6) zenye thamani ya shilingi za kitanzania Millioni Kumi na tano (15,000,000) Kwa Askari wa Uhifadhi wa TAWA kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria katika Pori la Akiba Maswa. Akimkabidhi Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Mlage Kabange msaada huo katika Ofisi za Makao  Makuu ya TAWA zilizopo Mkoani Morogoro Oktoba 31,2024, Captain Willness Minja kwa niaba ya Kampuni ya Bushman amesema wamekabidhi vitendea kazi hivyo kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria katika Pori la Akiba Maswa wao kama miongoni mwa wadau wakubwa wa uhifadhi katika hifadhi hiyo. Kwa upande wake, Kaimu Naibu Kamishna Kabange ameishukuru Kampuni ya Bushman kwa ufadhili huo ambao unalenga kuimarisha usimamizi wa shughuli za uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori. "Tunashukuru sana wawekezaji wetu

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na Wakulima, Wafugaji, Mamlaka za wanyamapori , Mamlaka za maji na Afya waendelee kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalamu katika sekta husika ili kujiepusha na athari za mvua zinaponyesha. Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 31,2024 Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia  Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili 2025. Amesema kuwa, mvua za msimu ni mahususi katika maeneo ya Magharibi mwa nchi Kanda ya kati, Nyanda za juu kusini Magharibi kusini, ukanda wa  Pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambapo maeneo hayo yanapata msimu mmoja kwa mwaka. Aidha, kutokana na mifumo ya hali ya hewa, mvua za wastani hadi chini wastani zinatara
Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatarajia kuanza mradi mpya wa upelekaji umeme  vitongojini utakaohusisha ujenzi wa njia za kati na ndogo za kusafirisha umeme.  Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 31, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la Mhe. George Mwanisongole, Mbunge wa Mbozi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kupeleka umeme mkubwa kwenye Vitongoji ambavyo havijapata umeme mkubwa na hivyo kukosa sifa ya kuwepo kwenye miradi ya maendeleo.  "Kwenye mradi huu utakaoanza Desemba 2024 tumeboresha zaidi kwani tutakuwa na transfoma zenye ukubwa wa KVA 50, 100 na 200 kulingana na ukubwa wa Kitongoji." Amesema Mhe. Kapinga Ameongeza kuwa, maeneo ya Vitongoji ambayo hayakunufaika na mradi wa awali wa vitongoji 15 yatanufaika kwa mradi utakaoanza Desemba 2024. Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu aliyeuliza ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya umeme jazilishi maeneo ya Miji yenye sura za Vijiji kam

NAIBU KATIBU MKUU UCHUKUZI ATEMBELEA OFISI ZA TMA.

Image
Dar es Salaam, tarehe 30 Oktoba 2024. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Ndg. Ludovick Nduhiye amefanya ziara ya kutembelea ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zilizopo katika jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuzitambua Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Uchukuzi, kufahamu majukumu ya kiutendaji na kuelewa changamoto zinazowakabili na Mikakati ya kuimarisha Taasisi na utoaji wa huduma. Baada ya taarifa ya utendaji kutoka TMA, Naibu Katibu Mkuu, Uchukuzi aliipongeza TMA kwa kuendelea kuimarisha na kuboresha huduma za haki ya hewa nchini, ikiwemo kuongeza usahihi wa utabiri,  akieleza kuwa yeye ni mmoja wa wadau wa Mamlaka na anafuatilia, kuzingatia na kutumia taarifa za hali ya hewa. Kiuekweli taarifa zenu ni nzuri, niwapongeze sana TMA, mimi ni mdau wa taarifa zenu na nimekuwa nikizifuatilia, kuzizingatia na pia kuzitumia, naweza kusema TMA ya sasa si kama ile za zamani." Alisisitiza Ndg. Nduhiye. Aidha, akiwasilisha awali salamu

ACT WAZALENDO WATOA DOSARI HIZI ZOEZI LA UCHUKUAJI NA UREJESHAJI WA FOMU

Image
  Na Mwandishi wetu, Dar  Chama Cha ACT Wazalendo kimesema licha ya mazingira mazuri yanayotangazwa na Serikali kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa kuwa wa huru na haki lakini bado kuna mambo yanayoendelea ili kukwamisha vyama vya upinzani wasiweze kushiriki uchaguzi huo ambapo dosari kadhaa wamezibaini kwa baadhi ya maeneo ambapo wagombea wao wameenda kuchukua fomu . Akizungumza na waandishi wa Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti Bara ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita amesema katika baadhi ya maeneo wagombea wa ACT Wazalendo nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa  wametakiwa ili wapewe fomu ni lazima wapeleke vitambulisho vya uraia ili kuthibitisha uraia wao vinginevyo hawapewi fomu. “ Matukio kama haya yamejitokeza katika kata ya Kandawale, kijiji cha Mtumbei Mpopera kilichopo katika jimbo la Kilwa Kaskazini mkoani Lindi, zipo kasoro nyingi ambazo zimekuwa zikitokea katika hatua hii ya kuchukua na kurejesha fomu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa matukio haya hayatokei k

VIJIJI VYOTE NEWALA VIMEFIKIWA NA UMEME - MHE. KAPINGA

Image
Naibu Waziri Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Vijiji vyote 76 vya Jimbo la  ya Newala Vijijini Mkoa wa Mtwara vimefikiwa na huduma ya umeme kwa umbali wa kilometa 1.  Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la Mhe. Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala Vijijini aliyetaka kufahamu lini Serikali itaanza ujenzi wa nguzo za Kilomita 2 katika Vijiji ambavyo mradi wa  REA mzunguko wa Pili unatekelezwa. "Kwa nyongeza ya umbali wa kilomita 2, REA kupitia Mkandarasi Central Electrical International Limited anaendelea na kazi na amefanikiwa kufikisha umeme kwenye vijiji 32 kati ya vijiji 76. Vijiji vilivyosalia vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni", Amesema Mhe. Kapinga Akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Mhe. Abubakar Asenga aliyeuliza lini Serikali itaunganisha umeme katika Kitongoji cha Upendo, Tupendane, Ikwambi na Misheni katika mji wa Ifakara,  Mhe. Kapinga amesema vijiji hivyo vipo katika mradi wa vitongoji unaoendelea. Amesema

SERIKALI YAAHIDI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WABUNIFU WA MAJENGO

Image
Na Mwandishi wetu  Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kufanyia maboresho sera ya ujenzi ili kutengeneza sheria ya ujenzi itakayosidia  wataalamu wa wabunifu majengo na wakadiriaji ujenzi AQRB kufikia matamanio ya kukuza sekta ya ujenzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi duniani. Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Edward Mpogolo wakati akimuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Mashaka Biteko kwenye ufunguzi wa Mkutano wa  5 wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ambapo unafanyika kwa siku mbili. Amesema kuwa, mkutano huo uwapeleke kwenye tafakuri ya kuangalia changamoto walizopitia kwa kipindi cha miaka 5 na kuzifanyia kazi katika maboresho ili kuweza kupiga hatua zaidi kama Taifa na kwenda mbele kwenye ubunifu zaidi. Ameongeza kuwa, licha ya changamoto kubwa wanazozipitia lakini pia wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kusajili wabunifu 1586 huku 33 ndio wakitoka nje. Aidha, ametoa wito

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA MAGONJWA YA MLIPUKO

Image
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa rai kwa Viongozi wa Dini kote nchini, kutumia majukwaa yao kusaidia Serikali kutoa elimu sahihi ya kuepuka na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama Mpox, Kipindupindu na Marbug. Dkt. Mollel ameyasema hayo jijini Dar es Salaam  wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya  Jenista Mhagama kwenye Mkutano wa Waziri wa Afya na viongozi wa Dini kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko na suala la Bima ya Afya kwa Wote. Amesema viongozi hao wana wajibu wa kiroho wa kusaidia kuhakikisha wanailinda jamii na maradhi yanayoepukika kwa kutumia majukwaa yao ya ibada. "Tunazungumza nanyi kwa niaba ya waumini, viongozi wa dini kote nchini isaidieni Serikali kutoa elimu sahihi ya kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama Mpox, Kipindupindu na Marbug,"amesema Dkt. Mollel. Ameongeza kuwa jitihada za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendeleza jitihada za afua mtambuka ili kuhakikisha nchi inabaki salama. "Wakati tukifu

DKT. BITEKO AIPONGEZA REA UTEKELEZAJI MIRADI YA NISHATI

Image
Ni ya upelekaji umeme kwenye vijiji, vitongoji na Nishati Jadidifu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usambazaji umeme kwenye vijiji, vitongoji na usimamizi wa miradi ya Nishati Jadidifu ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya Wizara ya Nishati. Alitoa pongezi hizo tarehe 28 Oktoba, 2024 jijini Dodoma wakati wa kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ikiwa ni kikao cha pili toka uanzishwe mfumo  mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi. Katika kikao hicho, ilitolewa tathmini ya utendaji kazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara iliyofanyika katika kipindi cha miezi mitatu kinachoishia mwezi Septemba 2024 ambapo Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeongoza kwa kufanya vizuri ukifuatiwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

AQRB KUKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO, TEKNOLOJIA ZA KISASA KUTAMBULISHWA

Image
  Na Mwandishi wetu  Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakaddiriaji Majenzi (AQRB) leo itatoa taarifa ya bodi katika mkutano wake wa mwaka katika nyanja ya mafanikio pamoja na changamoto zilizojitokeza katika kipindi Cha mwaka moja uliopita. Aidha mkutano huo utafanyika katika  Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam ambapo kauli mbiu ni "Mabadiliko ya Teknolojia katika sekta ya ujenzi Tanzania" Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msajili wa wabunifu majengo na wakadiriahi ujenzi (AQRB) Mbunifu Majengo Edwin Nnunduma amesema katika mkutano huo watautumia pia   kutoa mafunzo endelevu kwa wataalamu wa masuala ya ujenzi. "Mafunzo hayo endelevu ya wataalamu yatafanyika kwa njia mbili moja ni maonesho kutakuwa na mabanda ya bidhaa na vifaa vya ujenzi,na pili kutakuwa na wataalamu"Amesema. Aidha Nnunduma amewaalika wananchi na wadau katika sekta ya ujenzi kuhudhuria katika mkutano wao ambapo watapat

DKT.BITEKO ATAKA UMOJA, USHIRIKIANO NA UBUNIFU TAASISI ZA NISHATI

Image
📌 *Asema Rais Samia anataka Ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi* 📌 *Asisitiza utendaji kazi umuangalie Mtanzania wa kawaida anayeitegemea Serikali kubadili maisha* 📌 *Aagiza kila Taasisi kuwa na Vigezo vya Upimaji Utendaji Kazi* 📌 *Ataka Watendaji waache alama ya kazi, si kulinda vyeo* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuwa na umoja, ushirikiano na ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi  ikiwemo za umeme, mafuta,na Nishati Safi ya Kupikia. Amesema hayo tarehe 28 Oktoba, 2024 jijini Dodoma wakati wa Kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ambacho ni cha pili kutoka uanzishwe mfumo  mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi. “Ikumbukwe kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wote amekuwa akisisitiza kuwepo na ubunifu kwenye Wizara na Taasisi ili ku

WADAU WA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WAKETI DAR, CDF, TAWLA WATOA NENO

Image
Na Mwandishi wetu Dar IMEELEZWA kuwa katika harakati za kumkwamua mtoto wa kike kuweza kupiga hatua kimaendeleo na kuzifikia ndoto zake, Serikali inajukumu kubwa la kutengeza mazingira salama na wezeshi ili kuhakikisha mtoto wa kike anapata haki sawa ikiwemo kuzuia ndoa za utotoni na kuruhusiwa kurudi mashuleni. Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa kushirikiana na Chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) wakisapotiwa na Shirika la Equality Now leo limewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ya Jamii ili kujadili sheria ya ndoa hasa kifungu cha 13 na 17 kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18. Katika mkutano huo wa mashirika yasiyo ya kiserikali CSO, wadau hao wataweza kujadili nini kifanyike katika mapendekezo kadhaa yaliotolewa na Mahakama kwenda kwa Serikali ikitaka sheria ya ndoa kupitia kifungu cha 13 na 17 ibadilishwe ili kumlinda mtoto wa kike asiweze kuolewa katika umri mdogo pamoja na kumlinda na madhara ya ndoa za utotoni. Koshuma Mtengeti ni Mkurugen

TUNAIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA MIUNDOMBINU YA NISHATI ILI KUFIKISHA HUDUMA KWA WOTE- DKT.MATARAGIO

Image
📌 *Asisitiza nia ya Serikali ni kutoa huduma stahiki bila kuangalia umbali au kipato* 📌 *Apongeza kampuni ya Puma Energy Tanzania kushirikiana na Serikali uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia* 📌 *Puma Energy Tanzania yaahidi kuendeleza ushirikiano* Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati,  Dkt. James Mataragio amesema Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji  na miundombinu ya Sekta ya Nishati nchini ili  kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma stahiki bila kujali umbali na vipato vyao. Dkt. Mataragio ameyaeleza hayo  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Mawakala na Wadau wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambayo  inaunga mkono juhudi za Serikali za kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia bidhaa za Puma Gas. Dkt. Mataragio amesema  moja ya majukumu ya Wizara ya Nishati ni kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma na watumiaji ili kuimarisha ushirikiano kati ya  sekta binafsi na Serikali utakaopelekea utoaji wa huduma bo

KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA KULETA UWEKEZAJI NA UBUNIFU MPYA TANZANIA -MHE. KADUARA

Image
📌 *Asema ARGeo-C10 itasaidia  Afrika kufikia suluhisho la upatikanaji Nishati Safi* 📌 *Awaita Washirika wa Maendeleo kuendeleza Jotoardhi Tanzania* 📌 *Dkt.Mataragio asema Tanzania imetumia ARGeo-C10 kutangaza hazina ya Jotoardhi* 📌 *Shirikisho la Jotoardhi Afrika (AGA) lasema ni Kongamano la aina yake* Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar, Mhe. Shaibu Kaduara amesema Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) lililofanyika nchini kuanzia tarehe 21 Oktoba 2024 litaleta uwekezaji na ubunifu mpya katika uendelezaji wa nishati ya Jotoardhi Tanzania. Mhe. Kaduara amesema hayo wakati hafla ya ufungaji wa kongamano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Oktoba, 2024. “Maarifa na utaalam uliopatikana katika kongamano hili utasaidia mustakabali wa Tanzania na Afrika katika kufikia suluhisho la upatikanaji wa nishati safi, kuongeza kasi ya maendeleo ya  jotoardhi Tanzania na kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji umeme.” A