AQRB KUKUTANA NA WADAU KUJADILI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO, TEKNOLOJIA ZA KISASA KUTAMBULISHWA
Na Mwandishi wetu
Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakaddiriaji Majenzi (AQRB) leo itatoa taarifa ya bodi katika mkutano wake wa mwaka katika nyanja ya mafanikio pamoja na changamoto zilizojitokeza katika kipindi Cha mwaka moja uliopita.
Aidha mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam ambapo kauli mbiu ni "Mabadiliko ya Teknolojia katika sekta ya ujenzi Tanzania"
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msajili wa wabunifu majengo na wakadiriahi ujenzi (AQRB) Mbunifu Majengo Edwin Nnunduma amesema katika mkutano huo watautumia pia kutoa mafunzo endelevu kwa wataalamu wa masuala ya ujenzi.
"Mafunzo hayo endelevu ya wataalamu yatafanyika kwa njia mbili moja ni maonesho kutakuwa na mabanda ya bidhaa na vifaa vya ujenzi,na pili kutakuwa na wataalamu"Amesema.
Aidha Nnunduma amewaalika wananchi na wadau katika sekta ya ujenzi kuhudhuria katika mkutano wao ambapo watapata fursa yakujionea na kuzitambua Teknolojia za kisasa ambazo zikitumika katika ujenzi zinaokoa gharama pamoja na muda.
Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Dkt.Boniphace Bulamile ameeleza kuwa kwenye mkutano huo mgeni rasmi ni Mkuu wa Mmkoa wa Dar es Salaam akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko.
Aidha Bulamile amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwasajili wataalamu wa ujenzi ambapo wataalamu wao wanazingatia aina ya jengo la kujengwa kulingana na ardhi ya eneo husika.
Hivyo, wadau mbalimbali wametakiwa kujitokeza katika mkutano huo ili kuweza kupata taarifa mbalimbali sambamba na kuongeza ujuzi mpya katika kazi zao za ujenzi.
Comments
Post a Comment