WADAU WA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WAKETI DAR, CDF, TAWLA WATOA NENO




Na Mwandishi wetu Dar

IMEELEZWA kuwa katika harakati za kumkwamua mtoto wa kike kuweza kupiga hatua kimaendeleo na kuzifikia ndoto zake, Serikali inajukumu kubwa la kutengeza mazingira salama na wezeshi ili kuhakikisha mtoto wa kike anapata haki sawa ikiwemo kuzuia ndoa za utotoni na kuruhusiwa kurudi mashuleni.

Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa kushirikiana na Chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) wakisapotiwa na Shirika la Equality Now leo limewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ya Jamii ili kujadili sheria ya ndoa hasa kifungu cha 13 na 17 kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18.

Katika mkutano huo wa mashirika yasiyo ya kiserikali CSO, wadau hao wataweza kujadili nini kifanyike katika mapendekezo kadhaa yaliotolewa na Mahakama kwenda kwa Serikali ikitaka sheria ya ndoa kupitia kifungu cha 13 na 17 ibadilishwe ili kumlinda mtoto wa kike asiweze kuolewa katika umri mdogo pamoja na kumlinda na madhara ya ndoa za utotoni.

Koshuma Mtengeti ni Mkurugenzi wa Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine wataangalia sera ya kumrudisha mtoto shuleni ambae amebeba mimba akiwa shuleni, ambapo watajadili kwa pamoja ni kwa namna gani watoto hao wataweza kusaidiwa ili wapate haki ya elimu. 



Akizungumzia suala la ukatili wa kingono ameeleza kuwa, takwimu zinaonesha asimilia 33 ya watoto wa kike wanapitia ukatili wa kingono ikiwemo mimba za utotoni na ndoa za utotoni ikilinganishwa na silimia 17 kwa watoto wa kiume .

Aidha, amesema katika maboresho ya ndoa, jambo la kwanza linaloonekana ni utayari wa kisiasa, mila na desturi ambapo hayo yote ni ya kuyafanyia kazi ili kumlinda mtoto wa kike, huku unyanyapaa ukishika kasi Pindi watoto hao wanaporudi mashuleni, pia hakuna mazingira rafiki ya wao kurudi mashuleni.

Kamati ya wataalam ya watoto wa Afrika inatoa mapendekezo kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya wanafunzi waliopata mimba wakiwa mashuleni ambapo inataka waruhusiwe kusoma bila kikwazo chochote.



Mkurugenzi wa Chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) na Mwenyekiti wa Mtandao wa kupinga ndoa za utotoni Itike Mwakimbile ameeleza wamekutana wao kama wadau kuangalia sera, mifumo na sheria zake zinazofanya kazi,ambapo ni kwa namna gani zinaweza ikabana sheria hizo ili kuzuia ndoa na mimba za utotoni.

Ameeleza kuwa sheria hizo zinaruhusu mtoto akiwa na miaka kati ya 14 na 15 kuolewa hivyo, wanafanya uchechemuzi kuangalia ni kwa namna gani sheria hizo zinaweza kuleta mabadiliko kutoka miaka hiyo hadi 18, ambapo kwa umoja wao watashirikiana kupaza sauti ili jamii kutambua madhara ya mimba za utotoni kwani madhara yake ni makubwa.

Rose Elisante ni Afisa program kutoka Shirika la Haki Elimu amesema licha ya kutoa semina kwa wadau kuhusu kuwa na uwelewa wakupokea watoto waliocha shuleni kutokana na kupata mimba lakini bado imeonekana suala hilo limegubikwa na changamoto kadhaa.



Muongozo uliotolewa juu wanafunzi walioapata mimba kurudi mashuleni umewapa nafasi maafisa elimu na walimu kuwapokea wanafunzi wanaorejea mashuleni lakini hali ya wanafunzi hao kunyanyapaliwa wanafunzi wenzao, kuitwa majina masiyofaa, mlolongo mrefu wa kuwataka wazazi kupitia wizarani imekua ni kikwazo cha baadhi yao kujikuta wanaacha tena shule.

"Hata zile sababu zilizowafanya wakatishe shule bado hazijafanyiwa marekebisho ikiwemo kutembea umbali mrefu, kukosa sodo kwa wanafunzi wa kike mashuleni, sisi kama wadau tunaendelea kutoa elimuna hamasa Kwa walimu na wanafunzikuweza kuwapokea ili waweze kusoma"

Mdau kutoka maendeleo ya Jamii ambae alishiriki katika mkutano huo Rogathe Loakaki amesema suala ya mtoto wa kike ni ajenda ya watu wote kwani wanatambua changamoto ni kubwa hivyo wao kama wadau watahakikisha maadhimio yatakayofikiwa wanayafanyia kazi ili kusukuma gurudumu hilo ili kumkwamua mtoto wa kike katika nyanja zote.





Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...