BONDIA AMIRI MATUMLA KUZICHAPA NA AMAVILA FEB 28

 


Na Mwandishi wetu 

Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba amesema kuwa pambano la knock out ya mama msimu wa tatu litanogesha na mapambano 12.

Aidha katika pambano la knock out ya mama msimu wa tatu bondia Amiri Matumla atazichapa dhidi ya mpinzani wake Paul Amavila kutoka Nchini Namibia. 

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam Zayumba amesema kuwa mapambano hayo yanatarajiwa kufanyika Februari 18 Mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Zayumba amebainisha kuwa katika usiku huo pambano kuu lolitakuwa ni la Bondia Amiri Matumla ambaye atapanda ulingoni katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni kuzichapa dhidi ya mpinzani wake kutoka Namibia, Paul Amavila.

Amebainisha kuwa Bondia Matumla katika pambano hilo atazichapa  na mpinzani wake huyo kwa mizunguko nane.

"Hili ni pambano lake la kwanza tangu ajiunge kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa na ameahidi kufanya vizuri kwa lengo la kuanza kutengeneza rekodi nzuri katika karia yake kupitia masumbwi," amesema Zayumba.

Zayumba ameongeza kuwa mapambano mengine 11 ya utangulizi yataongozwa na mkongwe Dullah Mbabe huku baadhi ya mabondia wengine watakaopanda ulingoni wakiwa ni Oscar Richard atakayezipiga na bondia kutoka Malawi.

Wengine ni Rashid Mtange kutoka Nacoz Camp chini ya kocha Ramadhani Uhadi 'Rama Jah' atazichapa na bondia kutoka India na  wengineo.

Amebainisha kuwa mapmabo hayo lengo lake ni kunadi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amefafanua kwamba Michezo wa ngumi katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt Samia,  umekuwa na mafanikio makubwa hivyo ni vema watanzania wakaendelea kumuunga mkono.

Aidha, amesema kuwa ,vingilio katika usiku huo wa Knock Out ya Mama Msimu wa tatu vitakuwa ni shilingi, 50,000, sh. 20000 na 10,000.

Naye Bondia Matumla, ambaye ni mtoto wa Rashid Matumla' Snake Man' amejinasibu kufanya vizuri pambano hilo kutokana na kupata maandalizi ya kutosha.

'Naomba watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia pambano hilo ambalo litakuwa na burudani ya aina yake, amesema.

Comments

Popular posts from this blog

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI