CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) KUTOA MAFUNZO YA MANUFAA YA UCHUMI WA BULUU KWA VIJANA
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa chuo cha Bahari Dar es Salaam Prof. Tumaini Gurumo amesema kuwa chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) kimeona kunafursa nyingi katika uchumi wa buluu hivyo kinatazamiwa kuanzisha mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa vijan kusiana na manufaa katika uchumi wa buluu.
Prof. Gurumo ameyasema hayo kwenye kongamano la uchumi wa buluu lilifanyika jiji Banjul nchini Gambia.
“Kweli katika kongamano hili tumakubaliana nchi zote za Afrika kutumia vyanzo vyetu vya maji kama vila bahari, mito mabwa, maziwa na vyanzo vingine kuhakiisha vinasaidia jamii za kiafrika hivyo sisi DMI tutaanzisha masomo kwa vijana kuonyesha fursa za Uchumi wa Buluu” Asema Gurumo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi Bi Stella Katondo amesema kuwa kongamo hilo limewakutanisha wataalam kutoka nchi zaidi ya kumi na Sita za Afrika ni muhimu sana kwa maendeleo na manufaa ya uchumi wa buluu. Hivyo kwa chuo cha DMI imepata nguvu ya kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa uchumi wa buluu.
Naye mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bi. Leticia Mutaki amesema kuwa kupitia kongamano hilo TASAC itaendelea na kazi ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika vyanzo vya maji ili viumbe walipo waendele kuishi kwa manufaa ya mazingira na wananchi.
Katika Kongamano lilifanyika kwa siku tatu liliwakutanisha wataalamu kutaka nchi zaidi ya kumi na sita walikubaliana kushirikiana katika kuweka nguvu ya pamoja kuona kwa namna gani vyanzo vya maji vilivyopo Afrika vina wanufaisha wanchi wote wa Afrika.
Comments
Post a Comment