HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DIWANI SHABANI KUHUSU MNADA WA PUGU,WADAU KUCHANGIA UJENZI WA OFISI
LICHA ya kufanya harambee kwa ajili ya kujenga ofisi ya wafanyabiashara wa Pugu Mnadani imeelezwa kuwa kuna Changamoto ya wafanyabiashara kupeleka ngo'mbe zao moja moja kwa moja kwenye machinjio bila kuzitisha kwenye Mnada hali inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya Mnada mkuu wa Pugu.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya harambee hiyo, jijini Dar es Salaam, Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni Shaban Mussa amesema kwa sasa mzunguko wa fedha umeshuka katika Mnada huo kutoka shill Bill 1.2 kwa siku hadi kufikia shill mill 800.
Amesema kuwa, kuna wafanyabiashara ambao sio waamini wanabeba mifugo kutoka mikoa mbalimbali hawaifikishi Mnadani na kupeka machinjioni moja kwa moja ambapo kisheria mifugo yote inatakiwa kufika mnadani hapo washushe ili wanunuzi wanunue na kwenda kuchinjwa machinjioni.
"Wanapopeleka ngo'mbe moja kwa moja machinjioni sisi hapa hatuwezi kupata fedha kwani sheria za machinjio haziruhusu kukusanya ushuru ngo'mbe zikiwa nzima, bali ni mifugo iliyochiniwa tu"amesema
Ameongeza kuwa, wameweka mikakati na mkuu wa minada pamoja na kuzungumza na viongozi wenzake kuhakikisha ngo'mbe zote zinazofika machinjio lazima zuwe na vibali ambayo vimesaini kutoka Mnada mkuu wa Pugu.
Aidha, amesema watakaa na wafanyabiashara kuwaeleza umuhimu wa kulipa kodi kwani changamoto zilizopo Mnadani hapo haziwezi kutatulika kama wao hawalipi kodi na maendeleo hayawezi kupatikana.
"Hapa tumesikiliza changamoto zao wanataka maji, barabara, taa lakini haya yote hayawezi kufanyika bila wao kulipa kodi, mapato yakikusanywa lazima maendeleo yaonekane"
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Pugu Mnadani Edward Ntemi amesema kuwa, kulichomsukuma kuanzisha harambee za ujenzi wa ofisi ya wafanyabiashara wa Pugu Mnadani na kushirikisha wadau ni changamoto za wafanyabiashara, ikiwemo kukosa sehemu maalum ya kukutana na kutatua changamoto zao kwa faraghaa, kwani kwa sasa wanakutana popote.
"Nilipochaguliwa mwaka 2024 niliahidi wapiga kura wangu nitafanya sherehe kuwa nitachinja ngo'mbe ili tule nyama lakini nikafikiria nyuma kwa hayyat Magufuli alivokuwa akifanya pesa za sherehe za uhuru akizihamishia kwenye ununuzi wa vitanda vya hospital, sisi hapa hatuna ofisi nikaona ni bora pesa hizi nizihamishie kwenye kwenye ujenzi wa ofisi" amesema Ntemi.
"Mfano mwezi unaokuja wa mfungo wa Ramadhani wageni wanaweza kufika na tukapewa tenda ya kusaply hata ngo'mbe 200 kama hatuna ofisi itakua ni changamoto.
Aidha, amewataka wadau mbalimbali waendelee kuwaunga mkono kwa kushirikiana na wanachama pamoja na viongozi wenzake wanamkakati wa kuanzisha vyanzo mbalimbali vya mapato, huku akiwataka wafanyabiashara hao kujiunga pamoja Kwa kujisajili ili wafahamike hata inapotekea jambo iwe rahisi kutatulika.
Naye, Meneja Mkuu wa Mnada Mkuu wa Pugu Noely Byamungu amezitaka Taasisi za kifedha kwenda kuekeza Mnadani hapo na kutoa elimu ya usimamizi wa fedha kwani fedha inayopatikana kwa siku Mnadani hapo ni kati mill 800 hadi Bill 1 lakini maisha ya wafanyabiashara hao hayaendani na mzunguko wa fedha hiyo.
"Mzunguko wetu wa fedha hapa ni mkubwa sana lakini maisha ya wafanyabiashara hapa hayaendani na uhalisia wa pesa wanayoipata kutokana na kukosa usimamizi mzuri wa fedha"
Comments
Post a Comment