KAMATI YA KITAIFA YA USIMAMIZI WA UANDAAJI WA MPANGO KAZI WA KITAIFA WAKUTANA DAR



Na Mwandishi wetu 

Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara imefanya kikao maalum kuhakikisha kuwa rasimu ya mpango kazi huo inakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa katika kulinda na kuheshimu haki za binadamu ndani ya mazingira ya biashara

 Aidha, pamoja na mambo mengine timu hiyo ya wataalam imekabidhi rasimu ya awali ya mpango kazi huo kwa kamati lengo ikiwa ni kufanya mapitio na kuidhinishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mohamed Khamis Hamad amesema kuwa, mpango kazi huo utakuwa na mikakati ambayo inahusiana na masuala ya haki za binadamu katika shuguhuli za kibiashara, Serikali baada ya kuridhia itaikabidhi wizara ya katiba na sheria ya Tanzania bara na Zanzibar kwa ajili ya kuratibu mchakato mzima.

Aidha, kikao hicho kimejumuisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia, na wataalam wa masuala ya haki za binadamu na biashara pamoja na makatibu wa kuu wa katiba na sheria kutoka bara na Zanzibar na Wizara ya fedha kutoka pande zote mbili. 

"Na tume ilianza kuratibu mchakato huo kwa kukusanya maoni ya watu wa haki za binadamu na biashara ikiwemo kwenye migodi, sekta ya nishati, tume ikatengeneza  tathimini ya haki za binadamu na biashara kwaajili ya kutengeneza rasmu ya mpango kazi wa haki za binadamu na biashara na kukabidhi kwa kamati ya kitaifa." amesema 

Amesema mpango kazi huo upo kwaajili ya maboresho na kufikishwa serikalini ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa taratibu zaidi mpaka kufikia 2030.  

"Tunaamimi serikali yetu inaonesha dhamira nzuri na nia nzuri katika mpango kazi huo wa kitaifa wa haki za binadamu na biashara kwa rasimu hiyo imefikia sehemu nzuri." amesema

Awali akizungumza wakati wa kikao, amepongeza juhudi za timu ya wataalam katika kuandaa rasimu hiyo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wote ili kuhakikisha kuwa mpango kazi huo unakuwa nyenzo madhubuti ya kuimarisha uwajibikaji wa makampuni katika kuheshimu haki za binadamu.

Baada ya mapitio ya Rasimu hiyo, wajumbe wa Kamati wamejadili kwa kina vipengele muhimu vya Mpango Kazi huo, huku wakitoa mapendekezo ya maboresho kabla ya hatua za mwisho za kuidhinisha na kuanza utekelezaji wake.

"Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara unalenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini kwa kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinazingatiwa ipasavyo katika shughuli za kibiashara, kulingana na Miongozo ya Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Haki za Binadamu." amesema Khamis

Comments

Popular posts from this blog

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI