RC CHALAMILA KUWAONGOZA WATANZANIA PAMBANO LA KNOCK OUT YA MAMA
IKIWA yamebaki masaa chache kushuhudiwa kwa mapambano kali la ngumi ambalo lilikuwa linasubirowa kwa hamu kubwa, imeelezwa kuwa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila anatarajiwa kuwaongoza Watanzania kushuhudia mapambano hayo ya ngumi yasiyokuwa ya kuwania mkanda yanayopigwa leo, Feb 28 katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni jijini humo.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana wakati mchakato wa kutambulisha mabondia watakaotwangana leo katika ukumbi huo, kwamba Mkuu wa Mkoa huo, Chalamila atakuwa miongoni mwa viongozi watakaokuwemo ukumbini humo kushuhudia mapambano hayo.
"Wakati tukiendelea 'Face Off' kwa mabondia watakaopigana (kesho), leo nimepata taarifa kuwa Mkuu wetu wa Mkoa anatufuatilia kupitia mitandao ya Kijamii ambayo ipo mubashara kwa sasa na ameahidi kuwepo kushuhudia," alisikika mmoja wa washehereshaji akisema.
Mchakato wa kutambulisha mabondia hao lililokwenda sanjari na tambo kutoka kwa mabondia ilisababisha bondia Abdallah Pazzy 'Dullah Mbabe' almanusura azichape kavukavu na mpinzani wake.
Awali kabla ya mchakato wa show face off kufanyika jioni ya jana Feb 27, 2025 mabondia hao walipata nafasi ya kupima uzito asubuhi huku wadau mbalimbali wakitarajiwa kuhudhuria pambano hilo lenye mvuto wa kipekee.
Pambano hilo linatazamiwa kwa hamu kubwa na kuvuta husia za mashabiki wengi ni kati ya mtoto wa Rashid Matumla Snake Man', Amiri Matumla dhidi ya Mnamibia, Pauls Amavila ambalo litakuwa 'Main Card'
Mkurugenzi wa Mafia Promotion, Ally Zayumba, akizungumza baada ya tukio hilo, amesema kutakuwa na mapambano 14 kwa mabondia wa ndani na nje ya nchi kuoneshana ubabe.
Ameongeza kuwa huo ni msimu wa tatu wanaandaa mapambano hayo 'Knockout ya Mama' lengo kubwa ni kuunga mkono juhudi anazofanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo na kunadi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
"Tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Dkt Samia kwa kutubeba katika michezo, wengi mmeshudia kuna goli la Mama, pia amefanya mengi katika sekta ya masumbwi nasi tunandaa mapambano haya ili kuunga mkono juhudi zake," amesema.
Comments
Post a Comment