MSHINDI WA KWANZA KUJINYAKULIA MILL 10, NGAO NA CHETI TUZO YA MWALIMU NYERERE
Na Mwandishi wetu
Tuzo ya kitaifa ya Mwalimu Nyerere ya uandishi wa bunifu itatolewa April 13 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa super Dome Masaki ambapo itahusisha mkusanyiko wa mashairi, tamthilia, hadithi za watoto na Riwaya .
Aidha, mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo atajinyakulia kitita cha shill mill 10, ngao pamoja na cheti na muswada wake utachapishwa na kusambazwa shuleni na kwenye maktaba za taifa, Mshindi wa Pili: Tuzo ya Shilingi Milioni 7 pamoja na Cheti, Mshindi wa Tatu: Shilingi milioni 5 na Cheti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hiyo, Prof. Penina Oniviel Mlama, amesema Kamati imetoa taarifa hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya hafla ya kilele cha utoaji wa tuzo hizo.
Aidha, Prof Mlama ameishukuru jamii ya wanahabari kwa mchango wao mkubwa katika kuitangaza Tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa katika mwaka wa fedha 2022/23.
"Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu leo imetangaza zawadi kwa washiriki watakaoshindana kuwania tuzo hiyo kwa mwaka wa 2024/25, itakayofanyika tarehe 13 Aprili 2025 katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam"
Ameongeza "Tuzo hii ni zao la juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na inaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania. Tumeingia mwaka wa tatu sasa tangu tuzo hii ianze kutolewa, na mwaka huu tumepokea mwitikio mzuri kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita,"Prof. Mlama.
Amesema kuwa, kwa mwaka huu, Tuzo hiyo imehusisha vipengele vinne vya uandishi ambavyo ni riwaya, hadithi za watoto, tamthiliya na mkusanyiko wa mashairi.
Sambamba na hayo, washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na hata kutoka nje ya nchi kama Czech Republic wamewasilisha miswada yao, na jopo la majaji limekamilisha kazi ya kuyapitia maandiko hayo na kuandaa orodha ya waliofuzu.
Prof. Mlama alibainisha kuwa orodha hiyo teule haionyeshi nafasi za ushindi, bali imepangwa kwa mpangilio wa alfabeti, na washindi watatangazwa rasmi katika siku ya sherehe.
Aidha, waandishi wa habari na umma kwa ujumla kuendelea kuiunga mkono Tuzo hii kwa kuitangaza na kushiriki katika hafla ya utoaji wa tuzo.
Comments
Post a Comment