OFISI YA CCM TAWI LA BUTIAMA YAZINDULIWA
Na Mwandishi wetu
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yeredi amezindua ofisi ya Chama cha Mapinduzi tawi la Butiama iliyopo kata ya Vingunguti ilikarabaitiwa na Mstahiki Meya wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo Mhe Omary Kumbilamoto.
Akizungumza mara baada ya kuzindua ofisi hiyo Chief Yeredi amempongeza Meya Kumbilamoto kwa kuweza kutimiza wajibu wake kama Diwani kwa kusimamia ujenzi hadi kukamilika kwa ofisi hiyo ikiwa ni mwendelezo wake wa kukarabati na kujenga ofisi za Chama ndani ya kata ya Vingunguti.
"Nimpongeza Diwani na Meya Kumbilamoto kwa jitihada zake hapa amesimamia ujenzi wa ofisi hii hadi kukamilika na hii sio hapa tu nimeona pia amefanya ukarabati mkubwa katika ofisi yetu ya CCM kata ya Vingunguti na maeneo mengine ya Chama" amesema Chief Yeredi
Nae Meya Kumbilamoto amesema lengo la ujenzi wa ofisi hiyo ni kuweka ustawi nzuri wa chama, na hiyo inatokana na kazi kubwa anayoifanya Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya kata ya Vingunguti kwani ameleta miradi mingi na yenye thamani kubwa ya fedha hivyo lazima tuboreshe mazingira ya ofisi za Chama ili kuendana na muonekano wa Vingunguti.
"Dkt Samia Suluhu Hassan mambo aliyotufanyia Vingunguti ni makubwa sana mji wetu zamani ulisahaulika ulikua kama mji wa kale lakini sasahivi miradi mikubwa na ya thamani inatekelezwa hivyo kama unapendeza basi na sisi lazima tuboreshe ofisi za Chama ili kuendana na mandhari ya mji wetu " amesema Kumbilamoto.
Comments
Post a Comment