STEVE NYERERE KUNOGESHA TAMASHA LA MTOKO WA PASAKA





Na Mwandishi wetu, Dar 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele maarufu kama (Steve Nyerere) ni miongoni mwa watu mashuhuri watakaohudhuria katika tamasha la mtoko wa Pasaka litakalofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Steve Nyerere amesema kuwa siku ya sikuu ya Pasaka kutafanyika tamasha kubwa la mtoko wa Pasaka ambapo litawakutanisha wasanii nguli wa mziki wa injili.

"Maombi yana nguvu kuliko mtutu wa bunduki,maombi yana nguvu kuliko matusi,maombi yana  nguvu kuliko kitu kingine chochote,hivyo siku hiyo tutaliombea Taifa na Rais Wetu Mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan "amesema

Ameongeza "sisi tumeona ndani ya mwezi huu(April)kulikua na mambo mengi ikiwemo ramadhani, kwaresma,na sasa tunelekea kwenye sikukuu ya Pasaka,hivyo kuelekea kilele cha sikukuu ya pasaka tutatoa pakeji ya vifaa vya kumsaidia mama mjamzito kujifungua katika Hospitali zote za Wilaya Mkoani Dar es salaam" 

Aidha, Steve amempongeza muimbaji  mkongwe wa nyimbo za injili Christina Shusho kwa kuandaa tamasha la mtoko wa pasaka litakalofanyika siku ya pasaka April,20,2025 katika ukumbi wa Superdome Masaki kuanzia saa saba mchana.

"Watakuwepo waimbaji wote nguli wa nyimbo za injili kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania Kenya,Uganda na kwingineko,ambapo  watashiriki katika tamasha hilo ambalo halitakua na kiingilio lenye kauli mbiu isemayo "kwa maombi utashinda"

Kwa upande wake Mwimbaji wa Nyimbo za injili Christina Shusho,amesema kwamba tamasha la "mtoko wa pasaka" linafanyika kwa mara ya tatu ambapo limelenga kuwaleta watanzania pamoja na raia wa mataifa mengine ili kufurahi kwa pamoja kupitia nyimbo na muziki wa injili. 

"Siku hii ni Maalum sana kwa ajili ya watu wote , hatuangalii dini wala kabila cha muhimu ni kuvaa na kupendeza, yaani  ukialikwa alikika"amesema Shusho.

Aidha, amesema waimbaji wengi watakutana na kufurahi lakini kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi pia watamuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazozifanya za kuliongoza Taifa la Tanzania ashinde katika uchaguzi.

Amesema kuwa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao imekua ikifanya mambo mengi ya kijamii,hivyo yeye kama mwanachama wa Taasisi hiyo ameamua kuandaa tamasha la nyimbo za injili siku ya sikukuu ya pasaka April 20,2025 ili kufurahi pamoja na jamii.

"Tumealika na watu mbalimbali ikiwemo ndani na nje ya nchi Kwa lengo la kujionea amani na utulivy uliopo nchini humo, huku wakifurahia burudani ya kutosha kutoka kwa wasanii nguli wa mziki wa injili".

Comments

Popular posts from this blog

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI