STEVE NYERERE - "NYUMBA ZA IBADA MUSIGEUZE GENGE LA SIASA"
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele (Steve Nyerere) amewataka viongozi wa nyumba za Ibada kurudi katika mstari wa kuhubiri amani na kuliombea taifa kwa maslahi mapana ya nchi .
Aidha, amesema nyumba za Ibada kwa sasa zimekua genge la kuhubiri siasa badala ya kumuomba Mungu ili watu wapate kupona kutokana shida zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo katika Ofisi ya Taasisi hiyo amesema kuwa, nyumba za Ibada zimekua zikitumia muda mwingi kutumia kuhubiri siasa badala ya kuhubiri amani kama ambayo tumezoea.
Amesema kuwa, ameamua kuzungumza hayo baada ya kuona viongozi wengi wa kiroho wamekua wakigeuza nyumba za Ibada kama genge la kuhubiri siasa jambo ambalo si jema kwa taifa la Tanzania.
Ameongeza kuwa, wanasiasa ni vyema kuhubiri siasa huko kwenye mikutano yao ya hadhara ili viongozi wa kiroho waendelee kutuvusha katika dhambi tulizonazo zipungue na waiombee Serikali na viongozi wetu wawe na maadili mema .
"Viongozi wa Kiroho warudi kama zamani kwani nyumba za Ibada ndio sehemu ya kupata amani ya moyo, tuna matatizo mengi ambayo yanahitaji kuombewa ili tupone, lakini ukiingia nyumba za Ibada sasa hivi kuswali dakika 5 mahubiri ya siasa dakika 70, hii sio sawa kabisa wanapotupeleka sio kila jambo na wakati wake"
Ameongeza "Tunalinda taifa letu kwa maslahi yetu wenyewe, tusikubali watu wachache watuharibie amani yetu, zamani kulikua na utaratibu wa kuombea viongozi wetu, wanafunzi, nchi yetu lakini sasa hivi huo utaratibu huo haupo tena, muda wote ni kuhubiri siasa".
Katika hatua nyengine ameipongeza timu ya Simba Sport Club kwa kuingia Fainal ya mashindano ya Afrika, huku akiwataka viongozi wa clab ya Simba na Yanga kutoruhusu watu wachache wasioitakia mema nchi ya Tanzania kuivuruga amani na kupoteza Ajira za vijana.
Comments
Post a Comment