WAKILI MADELEKA AJITOSA JIMBO LA KIVULE

Wakili Peter Madeleka leo amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia tiketi ya Chama cha Act Wazalendo . Mapema leo amefika katika katika Ofisi za Chama cha Act Wazalendo zilizopo Jimbo la Kivule Kata ya Kitunda, akiwa na wafuasi wa Chama hicho kuchukua fomu hiyo na kuomba ridhaa ya Chama hicho kumpitisha kugombea Jimbo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema ameamua kugombea Jimbo hilo ili kuweza kuwasaidia wananchi kutokana na changamoto nyingi za kijamii zinazowakabili Jimbo humo. "Jimbo hili ni jipya lakini hakuna maendeleo yoyote yaliyoletwa, barabara ni mbovu hazipitiki mvua zikinyesha mawasiliano yanakua shida, limesahaulika kwa muda mrefu sasa nimekuja mkombozi wao"amesema Wakili Madeleka Amesema kuwa, miongoni mwa ajenda zake atazokwenda nazo endapo chama kitampaa ridhaa ya kugombea katika Jimbo hilo ni kusimamia haki na kuhakikisha anaweka misingi mizuri ya watu kuishi bila maumivu. ...