Katibu wa Shina na mwanachama wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM,( UWT) Kigezi chini Kata ya Buyuni, Happyness Malya amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Udiwani wa Viti Maalumu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Amekabidhiwa fomu hiyo leo June 30,2025 na Katibu Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala
Makamu wa RAIS wa Seneti ya Jumuiya (SMAUJATA) shujaa wa maendeleo wa ustawi wa Jamii Fredrick Nelson Rwegasira amechukua fomu ya kutia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule. Rwegasira amechukua fomu hiyo leo Julai 1,2025 katika Ofisi za Katibu wa CCM Ilala Chief Sylvester Yaredi. Aidha amesema kwamba amejipima na kujitambua kua anafaa kugombea nafasi hiyo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kivule.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kipunguni Mwinjuma Abdul Seke amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule. Seke amekabidhiwa fomu hiyo leo June 30,2025 na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi. Aidha Seke amesema endapo atapata ridhaa ya kugombea katika Jimbo hilo atahakiksha anaunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluh Hassan za kuwaletea Maendeleo.
Comments
Post a Comment