KATIBU MKUU CHAUMMA APOKEA MAPENDEKEZO YA SIFA, VIGEZO VYA WANAWAKE WATAKAOTEULIWA UCHAGUZI MKUU
Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amewataka wanawake kujitokeza kuzigombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi mkuu kwani moja ya kigezo kitakachotumika kumpata kiongozi wa kiti maalum ni mchango wake wa kura kwa chama kwenye Uchaguzi mkuu.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akipokea mwongozo rasmi wenye mapendekezo ya sifa na vigezo vya wanawake wa chama hicho wanaotarajiwa kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi kupitia udiwani, ubunge na uwakilishi wa viti maalum katika uchaguzi wa mwaka huu.
Amesema kuwa, hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa chama kuhakikisha wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika uongozi, sambamba na kuzingatia uwiano wa kijinsia kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya chama na miongozo ya kitaifa.
Awali, Katibu wa Kamati Maalum ya Viti Maalum, Moza Ally amesema kuwa katika utengenezaji wa mwongozo huo wamezingatia sheria za uhaguzi, chama na Katiba ya Nchi ili kuhakikisha wanapata watu sahihi watakaoweza kuwatumikia wananchi watakaowaongoza.
Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwake na Katibu wa Kamati Maalum ya Viti Maalum, Moza Ally, aliyeteuliwa na Mwalimu mwenyewe kuongoza mchakato huo wa ndani kwa lengo la kuweka misingi madhubuti ya uteuzi wa wanawake wenye uwezo, maadili na uadilifu wa kutumikia wananchi kupitia vyombo vya uongozi.
Comments
Post a Comment