RAIS SAMIA KUZINDUA BANDARI KAVU YA KWALA NA UANZAJI RASMI WA TRENI YA MIZIGO YA SGR


Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (Mb), amesema kuwa hafla ya uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala na kuanza rasmi kwa safari za treni ya mizigo ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Dodoma itafanyika Julai 31, 2025, Kwala, mkoani Pwani, ikihusisha pia upokeaji wa mabehewa mapya na yaliyokarabatiwa ya reli ya zamani (MGR) ambapo Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa TPA Jijini Dar es salaam leo tarehe 25 Julai,2025 Waziri Mbarawa amesema Bandari Kavu ya Kwala, iliyojengwa Vigwaza, kilomita 90 kutoka Dar es Salaam, ina uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku (takribani 339,500 kwa mwaka), sawa na asilimia 30 ya makasha yote ya Bandari ya Dar es salaam na kueleza kuwa eneo hilo lilichaguliwa kutokana na jiografia nzuri na ardhi ya serikali isiyo na migogoro.

Ameongeza kuwa, treni ya mizigo ya SGR imeanza rasmi kutoa huduma kuanzia tarehe 27 Juni, 2025 baada ya majaribio kufanyika, ambapo imepunguza muda wa kusafirisha Mizigo  kutoka masaa 16 hadi masaa 4 kati ya Dar es Salaam na Dodoma na tayari makampuni kama Azania Group na Dangote Cement zimeshanufaika na huduma hiyo.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuboresha reli ya zamani (MGR) kwa kupokea mabehewa 50 mapya na 20 yaliyokarabatiwa ili kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo nchini na kukuza uchumi.

Faida zitakazopatikana ni pamoja na Kupunguza msongamano bandarini na barabarani, Kuongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam, Kupunguza ajali gharama za usafirisaji sambamba na kukuza ajira na biashara katika Mikoa jirani

Waziri ametoa mwito kwa wananchi na wadau wa usafirishaji kuhudhuria hafla hiyo na kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotokana na miradi hiyo muhimu kwa maslah ya Taifa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA Bw.Plasduce Mbosa amesema Mamlaka imejipanga kikamilifu kuhakikisha bandari ya Kwala inatoa huduma bora na za kiwango cha kimataifa 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mha Machibya Shiwa amesema TRC itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha huduma ya usafiri wa reli inaimarika nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI