RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU AMIRY AELEZEA MAFANIKIO YA MKUTANO WA UGANDA


Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Rajab Amiry amesema ameshiriki mkutano wa siku tatu nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine wamesaini makubaliano ya Muungano (MAU) kwa nchi zaidi ya 8 Afrika lengo ni kukuza tasnia ya Filamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es Salaam aliporudi katika mkutano huo uliofanyika nchini Uganda, amesema mkutano huo walijadili namna gani wanaweza kupata masoko makubwa hivyo wameweka utaratibu mzuri wa kusaini memorandam ambayo itasaidia filamu za Afrika kuweza kuwa katika sehemu nzuri.











"Tunashukuru Serikali ya Uganda ambayo ilikuwa sehemu ya udhamani, UNESCO kwa ajili ya kufadhili, Tanzania kwa kutuamini kwa kuwepo bodi ya filamu kuwakilisha, Zanzibar nayo ilikuwepo katika mkutano huo" amesema Rajab

Hata hivyo, amesema kushiriki katika mkutano huo kumezaa matunda ya kukutana na Marais wengine wa Shiriko Afrika ambapo imepelelekea kufungua milango mingine katika filamu haswa kwa waigizaji nchini hivyo wajiandae kupata matunda mazuri.

Naye, Afisa filamu Ally  Makata  aliongezea lengo kubwa kama bodi ya filamu ni kuhakikisha wanaleta maendelea katika tathnia ya filamu na michezo ya kuigiza 

"Ikumbukwe kuwa michezo ya kuigiza na filamu imekuwa biashara na ajira kwa watu wengi hivyo ikatufanya tushiriki mkutano huo ili kuwepo na makubaliano ambayo ni kujenga uwezo na masoko na yaliyozungumzwa ni yale ya ( Streem East) itakuwa app ambayo lenye lengo la kutengeneza kazi zenye ubora kwa wasanii ilikuweza kupata masoko nje na ndani ya Afrika" amesema Makata

Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zaidi ya nane ambazo ni Tanzani,  Uganda, Kenya, Ethiopia, Malawi,Zambia, Rwanda.


Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Godliva Godrian amesema walitaka kujua wenzao wanafanya vipi ili kukuza Filamu zao katika Masoko ya biashara hivyo wameungana nao ili wapate kuungana na kushirikiana kwa pamoja ili kukuza filamu katika soko la kimataifa.

"Tukiwaangalia wenzetu kama Korea,China  wamekua kwa kiasi kikubwa katika soko la biashara kwa sababu waliungana na kushirikiana" amesema makamu 

Ametoa rai kwa Tanzania kuendelee kushirikiana wao kwa wao na kujiaminisha kama wanaweza na huko wanapokwenda ni kwa ajili yao.



Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI