VETA MTWARA YAJA NA UBUNIFU HUU SABASABA
Chuo Cha Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) Mtwara kimeshiriki katika maonyesho ya sabasaba ambapo kinawaomba wazazi na walezi kuwapeleka watoto wai kushiriki katika maonyesho hayo ili waweze kufaidika.
Hayo yamebainishwa Julai 4,2025 Jijini Dar es salaam na Msanii mahili kutoka Chuo hicho Saidi Chilumba wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea bandi la VETA katika maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba
"Wewe kama ni mtengenezaji wa kitanda chonga na kinyago,ukiwa unasubiri mteja wa kitanda sasa unao uwezo mwingine wa mimsubiri mteja wa kinyago."amesema Chilumba
Hata hivyo, amesema kuwa Lakini pia wameongeza thamani kwenye vitu mbalimbali Kwa mfano tunatengeneza henga za nguo(Hooks) mafundi wa kuchomelea wanatupa baadi ya vipande vya chuma ambavyo wanaona wao havina thamani, kwahiyo sisi tunavigeuze tunatengeza structure kama ya kipepeo kama unavyoona,tumechora tingatinga."
Anasema fikiria kutoka shilingi 500 hadi elfu 25,tayari tumeshatengeneza fursa ya ajira kwa Vijana ambao walikua wanadhurula mitaani,wengine ambao hawajaenda VETA,tumewakusanya kwa ule ujuzi ambao tumeupata VETA tumekuaa tukiwapa Vijana hawa wajue zile bidhaa ambazo zilikua za kawaida sasa zimeanza kuwa ni thamani
Anasema Kipande hiki ukienda kwa fundi chuma ambaye amekipoteza ambapo ukienda kuuza inawezekana ukapata mia tano(500),lakini sisi baada ya kukiboresha kukiongezea thamani hii sanaa saivi tunauza elfu 25.
Comments
Post a Comment