VETA SONGEA YAWAFIKIA WATOTO SABASABA















Na Fatma Ally 

Chuo Cha Ufundi Stadi Songea (VETA) katika kuwa wabunifu kwenye maonesho ya 49 ya kimataifa imekuja na Kona ya watoto ambapo wataweza kujifunza vitu mbalimbali kupitia maonesho hayo.

Akizungumza na Matukio Daima Media Mwalimu Faulata Mutalemwa kutoka Songea alipokua katika maonyesho ya 49 ya kimataifa ya biashara amesema miongoni mwa mambo ambayo watoto wanaweza kujifunza ni pamoja stadi za mikono.

Aidha, amesema lengo la kuibua vipaji na kuwafundisha misingi ya maishakupitia kona hiyo ya watoto wanajifunza vitu mbalimbali ikiwemo stadi za mikono mbalimbali na kuondoka nazo.

Aidha ametaja stadi hizo amesema ni pamoja na ushonaji, urembo pamoja na masuala ya umeme.

"Kupitia kona ya watoto mtoto anaweza kujifunza vitu mbalimbali vya namna ya kuchana nywele, kutunza ngozi yake, namna ya kushona nguo zake pamoja na kudhiifadhi"amesema Mutalemwa.

Aidha ametoa wito kwa wazazi, walezi kutembelea katika Banda la Veta ili watoto wao waweze kujifunza vitu mbalimbali vinavyohusu maisha.

Hata hivyo, amesema watoto pia wanaweza kujifunza umeme namna ya gani taa inawaka huku akifuata hatua nyepesi.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MWINJUMA AUTAKA UBUNGE KIVULE