WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025






Na Mwandishi wetu

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutembelea mabanda ya maonesho ya pili ya huduma za kifedhanq kijamii 'Muharram Expo 2025' yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kiongozi Mwandamizi wa Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mohamed Issa, amesema  maonesho hayo ni ishara   ya kuingia mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni Muharram sawa na mwezi wa kwanza wa kiislamu Hijiria.

Amesema kuwa, katika maonesho hayo kutakua na mada mbalimbali ambazo zitatolewa kwa wananchi na wataweza kupata elimu kuhusu uwekezaji ambao hauna riba na watapata elimu namna ya kuweka akiba, kupata mikopo au uwezeshwaji usio na riba.

Pia amesema wananchi watapewa elimu kuhusu huduma za Masoko ya mitaji na dhamana na uwekezaji wa pamoja (Collective Investment Schemes) isiyo na riba kama vile mifuko ya Uwekezaji Halal au Halal Fund, hati fungani zisizo na riba inayofahamika kama Sukuk.

Aidha, katika Maonyesho hayo Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Selemani Jaffo, anatarajia kuwa mgeni rasmi, ambapo monesho hayo yameanza Julai 15, 2025 na yatahitimishwa baada ya siku saba huku yakijumuisha shughuli mbalimbiali za kifedha zisizo za riba kama huduma za kibenki, vicoba na Saccos.

Vile vile watapewa elimu kuhusu hisa za kampuni, zilizokidhi masharti ya Shari'ah hivyo kuwa Halal na namna ya kujichunga na hisa zisizo Halal, pia watapewa huduma za kifedha na maelezo ya huduma za kijamii kama vile uwekaji wa wakfu, huduma za afya kutoka kwa jopo la madaktari.

Kwa upande wake, Amiri wa Baraza Kuu la Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha, amesema kuwa maonesho hayo si kwa ajili wa waislamu pekee bali ni kwa Watanzania wote bila kujali dini.

"Maonesho haya hayajachagua dini maalum ndio maana tumeyaweka katika viwanja vya wazi ili kila mwananchi afike kupata huduma hususani wafanyabiashara ambao wameathirika na mikopo ya kausha damu hivyo watapata elimu sahihi kuhusu mikopo," amesema Sheikh Kundecha.

Hata hivyo, amesema katika maonesho hayo kutakuwepo uchangiaji wa damu kwa hiari, huduma za msaada wa kisheria kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria hivyo, wananchi ni muhimu kufika ili kuweza kupata taarifa ya masuala mbalimbali.

Naye, Hassan Mohamed Issa kutoka Kampuni ya  Yusra Sukuk amesema wameshiriki katika maonyesho hayo kwa kutoa huduma mbili ya Yusra Sukuk na Yusra Takaful ambapo Yusra Sukuk ni uwekezaji wa hatifungani halali ambao unawekeza bila na riba.

"Sisi tupo hapa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi namna watakavyoekeza mali zao bila kufungamana na riba yoyote kama uwekezaji mwengine unaoekeza katika Taasisi nyengine"amesema Sheikh Hassan.

Amesema kuwa, Yusra Takaful ni mfuko wa bima ambao unafata misingi ya kiislamu ambapo mwananchi anajiunga bila kufungamana na riba yoyote"

Ameongeza."mtu anaweza akakata bima na asilimia 50 ya bima yake ikaingia kwenye Takaful Fund ambayo inakwenda kufanyiwa shughuli halali za kijamii na kuingiza kipato na baadae yule mtu anapata faida" .

Hata hivyo, amewataka wananchi kujitokeza katika mabanda hayo ili kupata elimu ya uwekezaji katika mfuko halali ambao hauna bima wa Yusra Sukuk na Yusra Takaful.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI