WMA YATOA WITO HUU KWA WANANCHI
WANANCHI wametakiwa kuuliza na kujiridhisha wanapokwenda kupata huduma kama bidhaa wanazouziwa vimehakikiwa na Wakala wa Vipimo Tanzania ili kuhakikisha wanapata stahiki zao.
Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano Wakala wa Vipimo Tanzania WMA Veronica Simba alipokua akizungumza na Mtandao wa Habari Plus katika maonyesho yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Sabasaba.
Amesema kuwa, kupitia maonyesho hayo wamejifunza vitu vingi sana licha ya kuona mwitikio mkubwa wa wananchi lakini wamegundua wananchi hawana uthubutu wa kuuliza maswali ya uhakiki wa Vipimo wanapokwenda kupatiwa huduma.
"Tumegundua kwamba wapo hata wale wanaofahamu kuhusu vipimo lakini bado wana uwoga hawana uthubutu wa kuliza kama je kipimo kilichotumika kutoa huduma kimehakikiwa na Wakala wa Vipimo ?"amesema Veronica.
Hata hivyo, amesema ni haki ya kila mwananchi, mlaji au mdau wa vipimo kujiridhisha na anahaki ya kumuliza mtoa huduma kama bidhaa anampatia imehakikiwa na akuonyeshe stika ya wakala wa vipimo.
Amesema kuwa, wakala wa vipimo wamekua wakihusika kwenye sekta zote zinazohusiana na vipimo ikiwemo mita za jami, miundombinu, mafuta na gesi Afya na endapo utabani hakuna stika ya wakala wa vipimo unatakiwa upige simu bure.
"Ukiona hakuna stika tupigie simu sisi tupo Tanzania nzima tutatuma wakala wetu atakuja kujiridhisha na kukusaidia kutokana na hiyo changamoto pia sehem kama vituo vya mafuta tunahakiki vipimo unapokwenda kupata huduma kwenye chombo chako, iwe pikipiki gari, bajaji jiridhishe je mkonga umehakikiwa una stika ya wakala wa vipimo"
Comments
Post a Comment