JESCA MOTTO AAHIDI MAKUBWA BUYUNI
Mgombea wa Udiwani Kata ya Buyuni Jimbo la Ukonga, Jesca Motto, amesema atahakikisha Kata hiyo inapata maendeleo makubwa chini ya uongozi wake kutokana na kuguswa moja kwa moja na changamoto zilizopo ndani ya Kata hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi kwa nafasi hiyo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Chief Sylvester Yaredi katika Ofisi za CCM wilaya ya Ilala amekishukuru Chama chake kwa kumpitisha .
"Ulikua mchakato mgumu wagombea walikua wengi lakini nashukuru Chama changu kwa kunipitisha nikawakilishe wananchi naahidi nitatatua changamoto zilizopo katika Kata yetu, tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha maendeleo yanapatikana"amesema Jesca Motto.
Aidha, amesema amemua, kuchukua fomu ya kuomba kugombea udiwani Kata Buyuni ili aweze kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amevutiwa sana na uongozi wake wa kuwatumikia wananchi .
"Nitajitolea kwa wananchi wangu kuhakikisha wanapata maendeleo katika sekta zote muhimu ikiwemo Afya, Maji na Elimu, nimechaguliwa kuwatumikia wananchi na nipo tayari kujitolea,mimi ni mwakilishi wao, Serikali imejitahidi kutuletea mahitaji mengi kwa ajili ya jamii lazima na sisi tuisaidie kuleta maendeleo".
Comments
Post a Comment