Mgombea udiwani katika Kata ya Liwiti kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ), Alice Mwangomo, ameeleza mikakati yake ya kuibadilisha kata hiyo endapo atapata ridhaa katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza leo Agosti 15,2025 jijini Dare es Salaam mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Sylivester Yaredi, amekishukuru chama hicho kwa kumuamini tena kwa mara ya pili kupeperusha bendera katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Chama Cha Mapinduzi imefanya mambo makubwa mwaka 2020 - 2025 kwa kutatua changamoto za wananchi wa Kata ya Liwiti ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari kwa mtindo wa ghorofa
"Kata ya Liwiti haikuwa na shule ya sekondari lakini kutokana na juhudi za chama chetu na Serikali imeweza kutatua changamoto ya shule ya sekondari, madaraja yanayounganisha Kata ya Kimanga, Kisukuru na Segerea," amesema Mwangomo.
Comments
Post a Comment