MGOMBEA UDIWANI PUGU STESHENI AAHIDI KUTEKELEZA ILANI
Mgombea wa udiwani kata ya Pugu Stesheni kupitia Chama Cha mapinduzi Salumu Shaibu Omary amewaahidi wananchi wa kata hiyo kuwafanyia kazi kwa bidii na kuhakikisha ilani ya chama hicho inatekelezwa ipasavyo.
Ameyasema hayo leo August 25 jijini dare es salaam baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi na katibu wa ccm wilaya ya ilala chief Sylvester Yared, ambapo amesema atafanya kazi kwa bidii ili kutatua kero zilizopo katika kata hiyo ya pugu stesheni.
"Nawashukuru wajumbe kwa kuniteua naahidi nitafanya kazi kwa bidii na kutatua kero za wananchi wa kata ya pugu stesheni amesema Omary"
Comments
Post a Comment