LUCY AWATAKA WANANCHI KUIUNGA MKONO CCM



 Na Mwandishi Wetu 

MGOMBEA wa udiwani wa Kata ya Kisukuru kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),  Lucy Lugome, ameahidi kuendesha kampeni za kistaarabu, zenye amani na busara, huku akiwataka wakazi wa Kisukuru kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono CCM katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 29 mwaka.huu.

Lugome ambaye anagombea kwa kipindi cha pili katika kata hiyo  ameyabainisha hayo leo Agosti 15, 2025 Jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea rasmi barua ya uteuzi  kwa ajili ya kupeperusha bendera katika Uchaguzi Mkuu .

“Nitaendesha uchaguzi wa amani, hekima na busara kwa lengo la kupata kura za kishindo kwa Rais wetu wa Tanzania, wabunge na madiwani,” amesema Lugome 

Ameongeza kuwa, Kata ya Kisukuru iko katika mikono salama chini ya uongozi wake na kuanzia sasa, wananchi wote wamekubaliana kwa pamoja kuacha makundi ya kiushindani na kuungana katika jitihada za kuhakikisha ushindi wa CCM.

“Kuanzia leo na kuendelea, sisi watu wa Kisukuru hatuna makundi. Tupo tayari kukitafutia kura Chama cha Mapinduzi kwa kishindo,” amesisitiza  Lugome.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI