KANIKI AAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI ZINGIZIWA

 



Na Mwandishi wetu

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Zingiziwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Selemani Kaniki, amekishukuru  Chama hicho kwa kumpa ridhaa ya kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2025, mara baada ya kupokea barua rasmi ya uteuzi, katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala, Kaniki amesema uteuzi huo ni heshima kubwa kwake na kwa wakazi wa Zingiziwa ambao amewahakikishia utumishi uliotukuka.

“Nakishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kuniamini na kuniteua rasmi kuwa mgombea wa udiwani wa Kata ya Zingiziwa. Hii ni furaha kubwa na ndoto niliyoiombea kwa muda mrefu kwa ajili ya kuwatumikia Wanazingiziwa,” amesema Kaniki.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI