MAKUYUNI WILDLIFE PARK YAZIDI KUWAVUTIA WAGENI WA KIMATAIFA


Na Mwandishi wetu, Arusha

Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park iliyo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA inaendelea kujidhihirisha kama lulu mpya ya utalii nchini  hususani katika ukanda wa kaskazini, ikiwavutia wageni wa ndani na nje ya nchi kwa mandhari yake ya kipekee na utajiri wa wingi wa idadi na spishi mbalimbali za wanyamapori.

Leo Septemba 8, 2025 hifadhi hiyo imepokea tena kundi la wageni wa kimataifa kutoka mataifa mbalimbali kupitia kampuni maarufu ya utalii, Ranger Safaris & Tours, yenye makao yake jijini Arusha.

Zaidi ya wageni 20 kutoka Denmark, Australia na New Zealand wametembelea hifadhi hiyo na kueleza kufurahishwa kwao na mandhari ya kipekee, urithi wa kiasili na vivutio adimu vinavyopatikana hifadhini humo.

Aidha,  Wageni hao wameeleza kuridhishwa na ubora wa Makuyuni Wildlife Park na baadhi yao wakaahidi kurejea tena Novemba mwaka huu kwa ziara ya pili.

Wakizungumza mara baada ya kutembelea hifadhi na kujionea vivutio , wageni hao pia wameahidi kuitangaza Makuyuni Wildlife Park katika masoko ya kimataifa, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza umaarufu na kuhamasisha wageni zaidi kuitembelea.

Makuyuni Wildlife Park, iliyopo eneo la Makuyuni mkoani Arusha inazidi kujitokeza kama moja ya hifadhi mpya zenye fursa kubwa za kukuza utalii nchini zinazokua Kwa kasi katika viwango vya ubora wa kuwaridhisha wageni wa hadhi ya juu.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MWINJUMA AUTAKA UBUNGE KIVULE