MRADI WA TAZA KUFUNGUA SOKO JIPYA LA BIASHARA YA UMEME AFRIKA
Wafikia asilimia 83 Dkt. Mataragio akagua mradi na kutoa maelekezo TANESCO TAZA kuunganisha Mkoa wa Rukwa na gridi ya Taifa Kuimarisha upatikanaji umeme Mikoa ya Kusini mwa Tanzania Mbeya Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Zambia kupitia Tunduma (TAZA) umefikia asilimia 83.45 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 2026 na hivyo kufungua soko jipya la biashara ya umeme barani Afrika. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo leo Oktoba 23, 2025 katika eneo la Iganjo, Mbeya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema mradi wa TAZA ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa utaiunganisha Tanzania na Nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool) na pia kuimarisha muunganiko wa ukanda wa Mashariki mwa Afrika (East Africa Power Pool). “Nimshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati. K...