WAMAMA 137 WANUFAIKA NA ELIMU YA POLIO HOSPITALI YA RUFAA MWANYAMALA

 



Na Mwandishi. Wetu --Dar es salaam

Ikiwa zimesalia siku kadhaa Tanzania kuungana na nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya Polio duniani Oktoba 24, 2025, klabu ya Rotary Mikocheni imetoa hamasa kwa wakina mama 137 kuhakikisha wanapojifungua watoto wao wanapata chanjo zote ikiwemo ya Polio wanapofikisha miezi 6 ili wawe salama.

Ameyasema hayo Oktoba 2025, Rais wa Klabu ya Rotary Mikocheni Nasibu Mahinya katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala jijini Dar es salaam wakati wakihamasisha wakina mama kuhudhuria kliniki mara baada ya kujifungua ili watoto wao wapatiwe chanjo zote kuwaepusha na magonjwa yanayoweza epukika ikiwemo polio.

"Hii ni wiki ya nane ya kampeni ya ‘Mama, Mkinge Mwanao!’ ambayo klabu ya Rotary tumeanzisha kwa kujitolea kuhamasisha wakina mama juu ya umuhimu wa chanjo ya Polio kwa wamama waliojifungua ili wahakikishe mara baada ya kuzaliwa watoto wao wanapata chanjo zote nne za Polio." Amesema rais Nasibu

Sambamba na hayo amebainisha kuwa Polio ni ugonjwa hatari unaosababisha kupooza na kusabisha mtoto kushindwa kutembea hivyo amewasisitiza wakina mama kuhakikisha wanafika vituo vya afya kupata chanjo kwani ni buree kabisa bila malipo.

Kwa Upande wake mhamasishaji wa kujitolea na mwanafunzi kutoka Chuo cha Kampala cha Tanzania Kennedy Munisi amesema kundi la watoto wachanga wanaozaliwa wako hatarini kupata ugonjwa wa polio, hivyo ndiyo maana Serikali inatoa chanjo bure za matone kwa watoto wachanga.

Pia ugonjwa huo unaambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na unashambulia mfumo wa hewa na chakula hivyo chafya kukohoa majimaji yakimpata mtu ambaye hujawahi kupata chanjo unaweza kumletea maambukizi.

Kampeni hii ya Mama, Mkinge Mwanao, inaendeshwa kwa ushirikiano wa klabu ya Rotary Mikocheni na klabu za Rotaract za Tanzania ikiwemo Rotaract klabu ya Kampala (KIUT).

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MWINJUMA AUTAKA UBUNGE KIVULE