Posts

Showing posts from June, 2023

ONESHO LA KWANZA LA EONII JUNE 23, MLIMANI CITY

Image
  Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar  Kampuni ya Azam Media Ltd (AML) kwa kushirikiana na Studio za PowerBrush (PBS) wanatarajia kuonesha  rasmi filamu ya Kisayansi ya EONII Juni 23, 2023 katika Ukumbi wa Century Sinemax Mlimani City Jijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Azam Media, Divisheni ya Maudhui na Utangazaji Yahya Mohamed amesema mipango yote muhimu imekamilika tayari kwa Onyesho hilo  la kwanza la uzinduzi wa kihistoria. "Tutumie fursa hii kwa niaba ya Azam Media Ltd na PowerBrush Studios kutambua mchango makubwa wa Serikali yetu katika kusimamia michezo na sanaa nchini na kuweka mipango endelevu ambayo tunashuhudia matunda yake kupitia mageuzi haya kwenye tasnia ya Filamu nchini,"amesema Mohamed. Aidha, amesema kuwa bodi ya Filamu wamekuwa mhimili mkubwa katika kutoa hamasa, kuratibu njia sahihi za kuisukuma sanaa ya Filamu na kipekee amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka chachu iliyop

DCEA YABAINI MBINU MPYA USAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA, WANAWAKE MATATANI

Image
  Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar  Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) imewataka wanawake nchini Tanzania kuwa makini wanapoingia katika mahusiano ya kimapenzi na raia wa kigeni ili kujiepusha kuingia kwenye matatizo ya usafirishaji wa madawa ya kulevya. Hatua hiyo imekuja mara baada ya mamlaka hiyo kumebaini mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambao huwatumia wanawake katika usambazaji wa dawa hizo bila wao kujua. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar er Salaam kamishna jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo amesema mbinu hiyo mpya wameigundua baada ya DCEA kufanya operesheni katika kipindi Cha miezi miwili na wiki tatu ambapo ilibaini wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakiwatumia wanawake kwa ajili ya kusafirisha dawa za kulevya. Amesema kuwa, hadi sasa jumla ya wanawake zaidi ya 20 wamekamatwa na tayari  wapo gerezani kutokana na kukutwa wakiwa wamedhihifadhi dawa hizo ambapo tayari wamefikishwa mahakamani na kes

REMBO AKABIDHI PIKIPIKI NA TOFALI 1000 IRINGA

Image
  Na Mwandishi wetu, HPMedia, Iringa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Iringa Injinia Fatma Rembo ambaye pia ni njumbe wa kamati ya utekelezaji wa UWT Taifa, leo amekabidhi pikipiki nne kwenye wilaya za mkoa wa Iringa ili kusukuma maendeleo. Hatu hiyo imekuja mara baada ya kufanya ziara katika wilaya za mkoa wa Iringa ambapo pamoja na mambo mengine pia amekabidhi Shilingi 1,000,000 kwa wilaya nne  kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za makatibu wa jumuiya hiyo. Akizungumza na wanachama wa UWT Mkoani humo, wakati wa kukabidhi pikipiki pamoja na fedha kwa ajili ya matofali amesema umoja na mshikamano katika chama chao ndio njia pekee ya kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake katika kumsaidia Rais wa JMT Dkt Samia Suluhu Hassan.  "Baada ya ziara yangu katika wilaya zote mkoani Iringa  niliahidi kukabidhi pikipiki na fedha kwa ajili ya matofali na leo nimetimiza , hivyo naomba tuendelee kumuunga mkono Rais wetu lwa kumsemea mazuri, pikipiki

UVCCM TAIFA - "HAWANA HOFU MASHIRIKIANO YA KUIMARISHA UCHUMI WA BANDARI"

Image
  Na Magrethy Katengu, HPMedia, Dar  Umoja wa  Vijana Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umesema Serikali inachofanya sasa ni mashirikiano ya Uwekezaji Bandarini ili kwenda kusaidia kuimarisha miundombinu ya bandari na shughuli nyingine za lojistiki na Uchukuzi ili Taifa liwe kitovu cha uchumi Imara. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Mohamed Kawaida, amesema kinachofanyika siyo maamuzi ya mtu binafsi bali ni maelekezo ya Chama kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kupitia ibara 22(1) Aidha amesema kuwa, kupitia uwekezaji ambao utafanyika utasaidia kuondoa urasimu na dosari zinazosababisha ucheweshwaji wa utoaji mizigo Bandarini. Hata hivyo, amesema licha ya kusambaa mizozo mitandaoni kuhusu bandari, katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 (a) inaeleza"kila mtu anao Uhuru wa kuwa na maoni ya kueleza fikra zake "hivyo wanaheshimu maoni ambayo yanatolewa na yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbal

ACT WAZALENDO YAISHAURI SERIKALI KUSHUSHA GHARAMA YA NISHATI MBADALA

Image
Na Mwandishi wetu, HPMedia  Chama cha ACT wazalendo kimeishauri serikali kuangalia namna bora ya kusaidia wananchi  wanaoshindwa kumudu gharama za kununua nishati mbadala ikiwemo gesi ili kusaidia uharibufu wa Mazingira. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Waziri Kivuli chama cha ACT Wazalendo Is-haka Mchinjita wakati akichambua bajeti iliyosomwa Jana Bungeni na Waziri wa Nishati January Makamba wameona katika kutekeleza hilo Serikali imetenga Shilingi bilioni 10 ruzuku ya  mitungi ya gesi na vifaa zaidi ya 200,000 Vijijini ili watumiw nishati mabadala ya kupikia na kusaidia kupunguza uharibifu wa Mazingira. "Serikali imekuwa kwenye mpango wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (Clean cooking) ambayo ni rafiki wa Mazingira na afya ya mwanadamu na inakadiriwa kwamba kila mwaka hekari milioni moja ya mita inakatwa kwa matumizi ya mkaa na Kuni na tayati matamko yametolewa yakisisitiza taasisinza umma na binafsi kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikap