Posts

Showing posts from July, 2023

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

WAZIRI PROF MKENDA AITAKA BODI YA MAKTABA KUEKEZA UNUNUZI WA VITABU.

Image
  Na Mwandishi wetu,  HPMedia, Dar  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameitaka bodi ya Maktaba kuwekeza zaidi kwenye ununuzi wa vitabu kuliko ujenzi wa majengo ya Maktaba kwani wanaweza kushirikiana na mashule kuanzisha maktaba za jumuiya. Kauli hiyo ameitoa Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitembelea ukarabati wa bodi ya huduma za maktaba ambapo amesema ni vyema kuwekeza katika ununuzi wa vitabu kuliko kujenga kwani kunachukua gharama sana. Aidha, amesema kuwa kuna changamoto kubwa ya uandishi na usomaji wa vitabu kutokana na wanaochapisha vitabu kukosa soko ambapo baadhi ya waandishi kutumia pesa zao kugharamia na wengine huacha kabisa.  "Zamani wakati ninasoma Maktaba zilikuwa nyingi kutokana na kuwekwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kanisani, misikitini na majengo ya Serikali hivyo niishauri bodi kutafuta maeneo ambayo wataweka vitabu ili kizazi cha sasa kuweze kusoma kwani kusubiri ujenzi wa Maktaba itachukua mda na kizazi cha sasa kitakosa kusom

TANZANIA YACHAGULIWA IPCC

Image
 Tanzania kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Ladislaus Chang’a, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, “Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC)”, katika Mkutano wa 59 wa IPCC (IPCC-59) unaoendelea katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 25 hadi 28 Julai, 2023. Dkt. Chang’a amechaguliwa katika nafasi hiyo katika uchaguzi wa viongozi wa IPCC (IPCC Bureau) uliofanyika tarehe 26 Julai, 2023. Wagombea katika nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti wa IPCC walikuwa jumla nane, kutoka Tanzania, Australia, Cuba, Eswatini, Germany, Hungary, Urusi na Afrika Kusini. Katika kinyang’anyiro hicho zilihitajika nafasi tatu na waliochaguliwa ni Tanzania, Cuba na Hungary. Aidha, Dk. Chang’a kwa kushirikiana na Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa IPCC waliochaguliwa katika Mkutano h

SERIKALI MBIONI KUZIFUTA KAMPUNI ZILIZOPITWA NA WAKATI

Image
TIPER YATOA GAWIO LA BILL 2.5 Na fatma Ally, HPMedia, Dar  Serikali inajipanga kuyafuta baadhi ya makampuni ambayo yamepitwa na wakati na kuyaunganisha ambayo yanafanyakazi zinazoshabihiana katika utoaji wa huduma kwa wateja baada ya kufanyika kwa uchambuzi wa kina ambao ritopi yake itakamilka mwezi ujao. Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Msaliji wa Hazina Nehemia Mchechu wakati alipokuwa katika hafla ya makabidhiano ya gawio la shill bill 2.5 kutoka kampuni ya Uhifadhi wa Mafuta Tanzania International Petroleum Reserves (TIPER) ambapo amesema lengo la Serikali la kuyaunganisha makampuni hayo ni kuleta tija zaidi. Aidha amesema kuwa, fedha hizo zilizotolewa na kampuni hiyo zitakwenda kusaidia katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, huku akifafanua kuwa, uchambuzi huo umeshafanyika kwa awamu ya kwanza na unaoendelea sasa hivi ni awamu ya mwisho ambao utakuja na majibu ambayo yatatangazwa baada ripoti ya uchambuzi huo kukamilika. Aidha, amesema lengo la uwekezaji ni kuon

KUTOKA KWA RAIS DKT SAMIA

Image
  Juma hili tumekuwa na mkutano na mjadala muhimu baina ya viongozi na wakuu wa nchi za Afrika kwa maendeleo na mustakabali wa nchi zetu na Bara letu, kuhusu Maendeleo ya Rasilimali Watu. Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuijalia nchi yetu fursa hii adhimu ya kukutanisha viongozi hawa katika nchi yetu kwa jambo hili lenye kheri na muhimu kwa maendeleo yetu. Mkutano huu umebeba kaulimbiu ya “Kuchochea Ukuaji wa Uchumi Afrika: Kuongeza Uzalishaji wa Vijana kupitia Mafunzo na Ujuzi’’, ajenda ambayo ndio moyo wa mataifa yetu – uwekezaji katika rasilimali watu, hususani vijana.  Mbali na kufikia azimio la pamoja (Azimio la Dar es Salaam) ambalo pamoja na mambo mengine litakuza ushirikiano wetu katika uwekezaji na maendeleo ya rasilimali watu, tumeshirikishana yale yanayofanyika katika nchi zetu. Sisi Tanzania tunaamini katika falsafa za waasisi wetu kuhusu umuhimu wa uwekezaji katika rasilimali watu ili kuleta maendeleo na uhuru wa kweli. Falsafa hizi bado zinaishi na ni sehemu ya dira

TANZANIA KUIWAKILISHA BARAZA KUU LA AFRIKA,UTALII DUNIANI

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ataliwakilisha Bara la Afrika katika nafasi ya Makamu wa Rais kwenye Baraza Kuu (General Assembly) la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).  Tanzania imepitishwa kwa kauli moja jioni ya jana Julai 26, 2023, katika Mkutano wa UNWTO Kanda ya Afrika kuliwakilisha Bara la Afrika na nafasi hiyo ya Tanzania itathibitishwa rasmi kiutaratibu tu (formality) kwenye Mkutano Mkuu wa UNWTO Oktoba mwaka huu mjini Samarkand, nchini Uzbekstan.  Kwa nafasi hiyo Waziri Mchengerwa atakuwa Makamu wa Rais wa Baraza hilo linalofanya maamuzi mengi makubwa duniani kuhusu utalii kwa niaba ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa kipindi cha miaka miwili.  Majira ya saa tatu usiku nchini Mauritius Tanzania imeshinda tena nafasi nyingine muhimu katika UNWTO ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu. Kamati hiyo ndiyo huchambua Bajeti na miradi ya kutekelezwa kabla haijapelekwa kwenye Baraza Kuu la UNWTO.  Nchi 13 za Afrika ziligombea na

AZAM TV KUPOKEA FILAMU ZENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA, YAZINDUA FILAMU MBILI

Image
Na fatma Ally,  HPMedia, Dar  Mkuu wa Chaneli ya Sinema zetu Sophia Mgaza amesema wanatarajia kuanza kupokea filamu hivi karibuni ambazo wanategemea kupata hadithi zenye utafiti wakutosha, uhalisia wa kitanzania na kugusa jamii na hadithi zenye stori ndefu isiyopungua dakika 90 na yenye viwango vya juu vya kimataifa inayoweza kuchezwa kwenye majumba ya Sinema pamoja na bajeti yake. Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na waandishi wa habari, wakati  Kampuni ya Azam TV kupitia chaneli yake ya Sinema zetu ilipokua ikizindua tamthilia mbili za moto ambazo ni Lolita na Mtaa wa Kaza moyo ambazo zinatarajiwa kuruka kuanzia tarehe 4 na 14 mwezi wa August mwaka huu chaneli 103. Aidha amesema tamthilia hizo zilizobeba simulizi za kuvutia si tu kwamba zinakuja kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini, bali zinaakisi maisha halisi ya Watanzania wa rika zote na zinahusisha waigizaji wenye vipaji na viwango vya juu. “Uzalishaji wa tamthilia hizi mbili Mtaa wa Kazamoyo

RAIS DKT SAMIA ASEMA AFRIKA INAHITAJI MAGEUZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Bara la Afrika linahitaji mageuzi katika nyanja zote muhimu kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akihutubia katika kilele cha mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu uliofanyika Jijini Dar es Salaam. "Ni wazi kuwa Bara letu bado linahitaji mageuzi makubwa katika nyanja zote muhimu za uzalishaji na maendeleo. Na haya ndio malengo na madhumuni ya ajenda ya Maendeleo ya Afrika tunayoitaka ya mwaka 2063 ambayo imeweka malengo 7", alieleza Mhe. Rais Samia. "Nataka nijielekeze kuyazungumzia malengo manne, ambayo ni Afrika ambayo mafanikio yake yanajikita kwenye ukuaji jumuishi wa uchumi na maendeleo endelevu, Bara lenye utangamano kisiasa kwa kuzingatia fikra za kimajumuishi na mwelekeo wa kimapinduzi, Afrika inayozingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria na Afrika ambayo maendeleo yake yanatokana na watu k

NCHI 43 ZASHIRIKI MKUTANO WA RASIMALI WATU AFRIKA TANZANIA

Image
Na Mwandishi wetu,Dar NCHI 43 za bara la Afrika  zashiriki mkutano wa Rasilimali Watu Afrika ambao unafanyika Tanzania kuanzia Julai 25 na 26 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.                                  Idadi hiyo ya nchi shiriki imetolewa na Benki ya Dunia (WB) ambao wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kuandaa mkutano huo muhimu katika eneo la rasilimali watu.          Kwa mujibu wa taarifa ambayo imesambazwa kwa waandishi wa habari imeonesha kuwa katika nchi hizo 43 zipo ambazo zimewakilishwa na Marais wenyewe, makamu wa rais, mawaziri wakuu, makamu waziri wakuu, mawaziri na watendaji wengine hii ni kuonyesha ushirikano ulipo baina ya nchi hizo .  Mkutano huo ulioanza Julai 25 ulifunguliwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ka ngazi ya mawaziri na watendaji wa nchi shiriki    Kabla ya mkutano huo kuanza Julai 24 walikutana watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi shiriki na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kus

WANANCHI WATAKIWA KUKUZA UCHUMI MKUTANONWA RASILIAMALI WATU

Image
  Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar  Imeelezwa kuwa kupitia mkutano wa kimataifa wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu  utakaofanyika Julai 25 hadi 26 jijini Dar es Salaam utasaidia kukuza pato la taifa na kuimarisha uchumi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa, mkutano huo ni matunda ni Rais Dkt Samia katika kuifungua nchi na kutangaza utalii  wa ndani hivyo kupitia mkutano huo kutakua na fursa na nyingi za kukuza uchumi. Amesema kuwa, mkutano huo utahudhuriwa na wageni 1200 kutoka katika nchi hizo ambao watakula na kulala katika holeti zaidi ya 40 ambapo wafanyabishara zaidi ya 100 wameshaandaliwa vizuri kuhusu bidhaa zao pamoja na uuzaji wao jambo ambalo litatoa fursa nyingi kwa hususani kwa watanzania ambao ndio wenyeji wa mkutano huo. "Kupitia ugeni huu watanzania hawana budi kutumia fursa hiyo kuweza kutangaza utalii wa ndani pamoja na kutangaza biashara zao, mahoteli, kupika vyakula vya

SUZA YAJA KIVINGINE "SOMA UJIAJIRI"

Image
Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar  Wazazi na walezi wameshauriwa kuwapeleka vijana wao katika chuo cha Taifa, (SUZA) ili waweze kujipatia elimu bora pamoja na maarifa yatakayo wawezesha kujiajiri wenyewe pindi wanapomaliza chuoni hapo. Akizungumza na waandishi wa habari leo July 18, Mkuu wa idara ya ujasiriamali wa chuo hicho, Dkt Moh'd Salim Ahmed wakati  walipotembelewa katika banda lao kwenye maonesho ya 18 ya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja yalioanza July 17 mwaka huu amesema kuwa kozi hiyo ni mpya chuoni hapo. Amesema kuwa,  katika chuo hicho wameongeza kozi mbili ikiwa ni pamoja na somo la ujasiriamali ambapo mpaka sasa wanafunzi wake wamekua wakifanya vizuri kwa  vitendo ikiwemo kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia mimea, ambapo kwa mwaka huu wanafunzi 19 watahitimu. "Hii kozi ni mpya lakini mpaka sasa tumeona matokeo mazuri kwa wanafunzi kwani wameweza kutengeneza vipodozi mbalimbali  kama vile lotion, Lipstic, mafuta p