SERIKALI KUONGEZA IDADI YA VIZIMBA ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA MAMBA KANDA YA ZIWA
Wananchi wapongeza jitihada za Serikali. Na Beatus Maganja SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi yake ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imetenga fedha zaidi ya shilingi milioni 210 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba saba Kanda ya Ziwa ili kuwalinda wananchi dhidi ya athari za wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba. Kauli hiyo imetolewa Oktoba 01, 2024 na Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga Katika ziara ya kukagua miradi ya vizimba na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vizimba hivyo kwa wananchi wa Buchosa, ziara iliyofanywa na TAWA wilayani humo. "Tunashukuru sana Kwa hii hatua ambayo imefanywa na Serikali ya kuongeza bajeti ya kujenga vizimba vingine, nimesikia bajeti hii tunayoendelea nayo imetengwa zaidi ya shilingi milioni 200 nyingine Kwa ajili ya kutengeneza vizimba zaidi ya saba " amesema Mhe. Seny