FURAHIKA YAWAFIKIA WAFANYAKAZI YAJA NA MPANGO HUU

Na Mwandishi wetu Wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na Chuo Cha Ufundi Veta Furahika kwa ajili ya masomo ya jioni kwa kozi mbalimbali Lengo la masomo hayo ya jioni kwa kundi hilo imeelezwa kuwa yanalenga kuwaongezea maarifa yenye tija yatakayoleta ufanisi katika majukumu yao ya kiofisi. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. David Msuya amesema kwamba masomo hayo yatawasaidia waajiriwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu ya kila siku na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea na yataendana mahitaji ya sasa. "Masomo haya ya jioni kwa waajiriwa wa Serikali na Sekta binafsi yataanza Machi 5, 2025 kuanzia saa 11 jioni hadi 1:00 usiku hivyo tunawakaribisha wote kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu," amesema. Dkt Msuya amezitaja kozi zitakazofundishwa chuoni hapo kwa muda wa jioni kuwa ni Public Administration (Utawala wa Umma), Human Resource Manag...