HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DIWANI SHABANI KUHUSU MNADA WA PUGU,WADAU KUCHANGIA UJENZI WA OFISI

LICHA ya kufanya harambee kwa ajili ya kujenga ofisi ya wafanyabiashara wa Pugu Mnadani imeelezwa kuwa kuna Changamoto ya wafanyabiashara kupeleka ngo'mbe zao moja moja kwa moja kwenye machinjio bila kuzitisha kwenye Mnada hali inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya Mnada mkuu wa Pugu. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya harambee hiyo, jijini Dar es Salaam, Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni Shaban Mussa amesema kwa sasa mzunguko wa fedha umeshuka katika Mnada huo kutoka shill Bill 1.2 kwa siku hadi kufikia shill mill 800. Amesema kuwa, kuna wafanyabiashara ambao sio waamini wanabeba mifugo kutoka mikoa mbalimbali hawaifikishi Mnadani na kupeka machinjioni moja kwa moja ambapo kisheria mifugo yote inatakiwa kufika mnadani hapo washushe ili wanunuzi wanunue na kwenda kuchinjwa machinjioni. "Wanapopeleka ngo'mbe moja kwa moja machinjioni sisi hapa hatuwezi kupata fedha kwani sheria za machinjio haziruhusu kukusanya ushuru ngo'mbe zikiwa nzima, bali ...