Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, ameungana na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini kushiriki hafla ya uzinduzi wa Ratiba ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara, kwa mwaka 2025. Uzinduzi huo umefanyika leo, Julai 26, 2025, katika ofisi za Makao Makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dodoma, na umeongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele. Tukio hili limeelezwa na viongozi mbalimbali kuwa ni hatua muhimu katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao, na linaakisi dhamira ya Tume ya Uchaguzi kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi yanatekelezwa kwa uwazi, ushirikishwaji na kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Akizungumza baada ya hafla hiyo, Katibu Mkuu wa NLD, Mhe. Doyo, alieleza kuwa chama chake kipo tayari kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Oktober mwaka huu. Alisema kuwa chama kimejipanga kusimamisha...