Mwanza, Geita Buseresere Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, akiendelea na kampeni zake Kanda ya Ziwa, amefanya mikutano ya hadhara katika Jimbo la Sengerema, eneo la Stendi ya Zamani, na Kata ya Buseresere, Mkoa wa Geita. Katika hotuba yake, Mhe. Doyo aliwataka wananchi wa Kanda ya Ziwa kutafakari kwa kina juu ya sababu zinazowafanya kuendelea kukosa maendeleo licha ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kushika dola kwa zaidi ya miaka 60. Mhe. Doyo aliwaahidi wananchi kuwa endapo watampa ridhaa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha wakulima wanapata fursa ya kuuza mazao yao katika masoko yenye tija na faida, badala ya kulazimishwa kuuza katika masoko yanayowanyonya na kuendeleza umaskini. “Wananchi, mkiniamini na kunipa kura Oktoba 29, nitasimamia na kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na zenye motisha kwenye mazao yenu yote. Haiwezekani mtumie gharama kubwa katika kilimo chenu halafu mpangiwe bei, hizi ni mbinu za kuendelez...