DKT.BITEKO AZINDUA MRADI UTAKAOWAKWAMUA VIJANA KIUCHUMI KATIKA MAENEO YANAYOPITIWA NA BOMBA LA MAFUTA GHAFI (EACOP)

Unahusisha kuongezea vijana ujuzi, kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha, na kuondoa vikwazo vya ujasiriamali na ajira binafsi Ataka ujuzi unaotolewa kwa vijana uende sambamba na utoaji wa mitaji Awaasa Vijana kuchangamkia fursa na kuwa waaminifu wanapopata nafasi Wanawake 6,130, Wanaume 4,905 na Makundi maalum 1,226 kufikiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amezindua Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE) ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa jamii zilizo karibu na miradi zinanufaika na miradi hiyo. Akizindua mradi huo katika Kijiji cha Bukombe, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita tarehe 18 Agosti 2025, Dkt. Biteko amesema mradi huo wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi ni moja ya miradi iliyopangwa kuwezeshwa na Kampuni ya EACOP kwa kipindi cha ujenzi na baada ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaj...