Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amegawa majiko 200 ya gesi kwa mama lishe wa soko la Machinga Complex lililopo Ilala Ili watumie nishati mbadala waache kutumia kuni katika kupika chakula . Akizungumza mbele ya mama lishe hao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema Rais wa Dkt Samia Suluhu Hassan anajali afya za wafanyabiashara wa mama lishe ndio maana amewagawia majiko Ili kurahisisha mapishi waache kutumia mapishi ya kutumia moshi ni hatari katika afya . "Tumegawa majiko ya gesi kwa mama lishe wa Ilala soko la Machinga Complex, Ilala Boma, Mchikichini na Gerezani, hii itawasaidia mama lishe kupika chakula na kupasha moto kila wakati kwa wateja wao itawavutia biashara zao "amesema Zungu . Aidha, amewataka waondokane na kasumba kwamba chakula ukipika na gesi sio kizuri badala yake watumie gesi katika mapishi yao mapishi ya gesi hayana moshi na chakula ki...