Posts

Showing posts from June, 2025

WANAOTAKA KUHARIBU UCHAGUZI MKUU WAONYWA, VIJANA WA CCM WACHARUKA

Image
Na Mwandishi wetu Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam wamewaonya wanasiasa na wanaharakati wanaohamasisha wananchi wasishiriki Uchaguzi Mkuu kwani ni dai la kikatiba na sio matakwa ya mtu binafsi. Akizungumza na  Waandishi wa habari Makao Makuu ya UVCCM Jijini Dar es salaam,mmoja wa Vijana hao Isack Sumbali amesema kuwa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi yamefanyika kwa kiasi kikubwa ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kubadilishwa nakuwa Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi(INEC). Amesema kuwa, tume miongoni mwa mabadiliko ni pamoja na kua na uhuru wa vyanzo vya mapato, ambapo awali ilikua haiwezi kujiendesha kwa fedha za ndani,na kutegemea ufadhili kutoka UNDP, ambapo uchaguzi mkuu wa mwaka huu utagharamiwa na fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha Sumbali amesema kuwa kwa sasa Uhuru wa Tume hiyo umeongezeka katika sehemu kuu mbili ambazo ni uhuru wa kitaasisi na uhuru wa kiutendaji,pamoja na kutungwa Sheria maalumu inayoongoza kupatikana kwa...

TANESCO YAWAPA SOMO WENYEVITI WA MITAA WILAYA YA KINONDONI NA UBUNGO

Image
Shirika la umeme TANESCO leo limekutana na wenyeviti wa mitaa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Ubungo lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa watendaji hao kwani shirika hilo asilimia kubwa utendaji unaanzia kwenye mitaa. Akifungua kikao kazi hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Altbert Chalamila  kilichoandaliwa na TANESCO kwa ajili ya Wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo amesema wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa kuwa miradi hutekelezwa katika maeneo yao. "Hata miradi mingi ya TANESCO iko kwenye mitaa hivyo, ni imani yangu kuwa kupitia kikao kazi hiki wenyeviti wote wanakwenda kuwa mabalozi wa kueleza huduma nzuri zinazotolewa na TANESCO pia kulinda miundombinu ya Shirika hilo"amesema RC Chalamila. Aidha ameipongeza TANESCO kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo muhimu ili liweze kufahamu kwa kina majukumu ya shirika hilo lakini pia kutoa mawazo na ushauri wa namna b...

DKT ABAS AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO

Image
  Dkt. Hassan Abbasi Ahamasisha Watanzania Kutembelea Tabora ZOO, Aahidi Maboresho Makubwa Zaidi ya Miundombinu. Na Mwandishi wetu, Tabora  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Juni 23, 2025 alifanya ziara katika bustani ya wanyamapori ya Tabora, maarufu kama Tabora ZOO, kwa lengo la kukagua na kuona usimamizi wa bustani hiyo ambapo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania hususani wa ukanda wa magharibi, wakazi wa Mkoa wa Tabora na Mikoa ya jirani kutembelea kivutio hicho cha kipekee ambacho kipo Katikati ya Mkoa wa Tabora. Katika ziara hiyo, Dkt. Abbasi ameonesha kuridhishwa na uwepo wa bustani hiyo ambayo ni hazina ya vivutio vya wanyamapori na mazingira asilia. Ameeleza kuwa Tabora ZOO ni sehemu muhimu ya utalii wa ndani ambayo Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya maboresho makubwa ya miundombinu ili kuvutia watalii wengi zaidi. "Hii ni Hifadhi ya kipekee, kuwa na eneo la heka zaidi ya 27 Katikati ya Manispaa ya Tabora au mji ni jambo k...

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MITAMBO 10 YA UCHORONGAJI KWA WACHIMBAJI WADOGO

Image
Asisitiza dhamira ya Serikali kuwainua wachimbaji wadogo kiuchumi Mitambo Yagharimu shilingi bilioni 12.41 STAMICO yasaini mkataba wa ushirikiano na VETA Dodoma, Katika mwendelezo hatua za Serikali kuendelea ya kuimarisha sekta ya wachimbaji wadogo nchini, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amezindua rasmi mitambo 10 ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo yenye thamani ya shilingi bilioni 12.41 iliyonunuliwa na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sambamba na vitendea kazi vya Shirika hilo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Shirika.  Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Juni 24, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa madini, wachimbaji pamoja na wananchi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuwawezesha wachimbaji wadogo il...

SEKTA YA NISHATI YACHANGIA ASILIMIA 14.4 YA PATO LA TAIFA

Image
Kapinga ampongeza Rais, Dkt. Samia kwa uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Nishati Aeleza mafanikio yaliyofikiwa katika Umeme, Gesi Asilia na Mafuta Asisitiza kuwa Nishati ni moyo wa uchumi Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Sekta ya Nishati ni moja kati ya Sekta tatu nchini ambazo zimechangia ukuaji wa pato la Taifa katika kipindi cha kati ya mwaka 2015 hadi 2025. Kapinga ameyasema hayo wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mipango na Uwekezaji Bungeni Jijini Dodoma.  "Mheshimiwa Mwenyekiti ukiangalia kwa tathmini kati ya mwaka 2024 hadi 2025 Sekta ya Nishati imefanya vizuri katika kuchangia pato la Taifa, Sekta hii imetoka asilimia 5.8 mwaka 2015 na sasa hivi tunazungumzia asilimia 14.4”. Amesema Mhe. Kapinga Ameongeza kuwa, Sekta ya Nishati imeweza kufanikiwa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanyika katika miradi ambapo  amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa uwekezaji huo mkubwa. "Katika Gesi na Mafuta y...

UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME NKANGAMO-MOMBA KUKAMILIKA MEI 2026

Image
Naibu  Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Nkangamo- Momba  unatarajiwa kukamilika Mei mwakani. Kapinga ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Momba, Condester Sichalwe (CCM) ambaye aliuliza ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha kusambaza umeme Nkangamo – Momba.  Kapinga amesema ujenzi wa kituo hicho cha Nkangamo - Momba ulianza mwezi Mei, 2024 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 30.

DKT MPANGO ATEMBELEA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA UZALISHAJI VIFAA TIBA NCHINI ITALIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametembelea Kampuni ya Kimataifa ya Uzalishaji Vifaa Tiba ya Health 3000 iliyopo Roma nchini Italia leo tarehe 23 Juni 2025. Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na viongozi wa kampuni hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Maurizio Flammini pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bi.Eleonora Flammini. Mazungumzo hayo yamelenga ushirikiano baina ya Tanzania na Kampuni ya Health 3000 hususani katika matibabu kwa njia ya mtandao (Telemedicine). Kampuni hiyo ni moja ya Makampuni yaliyo chini ya mwamvuli wa FG Group ambayo imejikita katika kutoa huduma za afya hususani uzalishaji wa vifaa tiba kwa kutumia teknolojia za kisasa. Makamu wa Rais yupo nchini Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Afrika na Serikali ya Italia (Mattei Plan) pamoja na mikutano mbalimbali ya uwili.

TANZANIA YAWA MFANO AFRIKA UTEKELEZAJI MIRADI SEKTA YA NISHATI

Image
Ufanisi wake watambuliwa Jukwaa la Nishati Afrika Lesotho kujifunza Tanzania utekelezaji miradi ya Nishati Mhandisi Mramba aeleza umuhimu wa Sekta Binafsi katika ukuaji wa Sekta ya Nishati Ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Nishati nchini ikiwemo ukamilishaji wa mradi wa usambazaji umeme katika Vijiji 12,318 umekuwa kivutio katika Jukwaa la Nishati Afrika linalofanyika nchini Afrika Kusini. Kutokana na ufanisi huo unaojumuisha ukamilishaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere wa megawati 2, 115 na baadhi ya miradi ya kikanda ya usafirishaji umeme, imepelekea nchi ya Lesotho   kueleza nia yake ya kuja Tanzania ili kujifunza masuala mbalimbali yatakayoboresha hali ya umeme nchini humo. Akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Nishati Afrika jijini Cape Town nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameeleza kuwa  Watanzania wanapaswa kujivunia jinsi Sekta ya Nishati inavyofanya vizuri na kuwa nchi ya mfano barani Afrika. "Wata...

MASHINDANO YA REDE YAZINDULIWA KATA YA PUGU

Image
Na Mwandishi wetu Dar  Mashindano ya Rede na mpira miguu yamezinduliwa Kata ya Pugu Station kwa kushirikisha timu 17 za  kata ya Pugu Station ikiwemo Pugu mpakani, kirumba, kibiriko na Msimbazi.  Akizungumza katika uzinduzi wa Rede Cup Afisa Mtendaji wa kata ya Pugu Station Iginas Maembe alisema jumla ya timu 14 zimeshiriki  Mashindano hayo yaliozinduliwa rasmi leo Juni 22/2025. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Afisa Mtendaji wa kata ya Pugu Station Iginas Maembe alisema dhumuni la Mashindano hayo kukuza vipaji na kujenga afya na Mahusiano kwani michezo ni afya . "Mashindano haya yanachezwa viwanja vya Mnadani na Bangulo ujumbe wa Mashindano haya mwaka huu"Tulithi mazuri tujenge kesho" dhumuni lingine kuwakumbusha wananchi nchi yetu inaelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka huu mwezi Octoba hivyo wananchi wajipange kuchagua viongozi sahihi watakaoleta maendeleo " alisema Iginas   Mtendaji Iginas Maembe alisema katika m...

FAINAL YA KOMBE LA JERRY SLAA CUP YAINGIA DOA, PURUKUSHANI ZA MASHABIKI, REFA AONDOLEWA UWANJANI KWA DIFENDA.

Image
  Na Mwandishi wetu Final ya mechi ya mpira wa miguu ya kombe la Jerry Slaa Cup Kati ya Mazinda na Shelaton United imehairishwa jana baada ya vurugu zilizotokea na kushindwa kufikia muafaka wa timu zote mbili. Awali timu ya Shelatoni ilishinda mabao mawili  katika kipindi cha kwanza cha dakika 45 huku timu ya Mazinda ikiambulia Sifuri. Kipindi cha pili dakika chache baada ya kurudi uwanjani timu ya Mazinda iliandika bao la kwanza jambo lililopelekea kusimama kwa muda kwa mchezo huo. Goli la kwanza lililofungwa na timu ya Mazinda lilikataliwa na timu ya Shelatoni United kwa madai kipa wao amechezewa rafu na kusababisha timu hiyo kugoma kuendelea kucheza. Wachezaji wote wa Shelaton United walitoka nje ya uwanjan na kushinikiza refa kukataa goli ili waendelee na mchezo, huku mashabiki wa timu hiyo wakitoa maneno makali kwa viongozi na refa. Tambo za mashabiki zilichukua muda, huku waliokua mbali na jukwaa kuu wakibaki njia panda wakisubiri hatma ya viongozi, mchezo huo ulisimama ...

WMA YAENDESHA ZOEZI LA UHAKIKI MITA ZA UMEME VIWANDANI

Image
DODOMA Wakala wa Vipimo (WMA) unaendesha zoezi la kuhakiki mita za umeme zilizofungwa katika viwanda mbalimbali nchini ili kuhakikisha Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inapata mapato stahiki na wenye viwanda wanalipa gharama stahiki kulingana na huduma ya umeme wanaotumia Hayo yalibainishwa Juni 18, 2025 na Meneja wa WMA Makao Makuu, Albogast Kajungu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika uwanja wa Chinangali, Dodoma. Kajungu alisema kuwa hadi sasa WMA imekagua mita za umeme zaidi ya 2,000 huku lengo likiwa ni kuhakiki mita zote zilizo kwenye matumizi katika viwanda vyote nchini katika zoezi lililoanza Mei mwaka huu. “Hali inaonesha kwamba mita nyingi zilizo kwenye matumizi viwandani ziko vizuri. Chache ambazo tumekuta zina mapungufu, tumewasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya kuzirekebisha na nyingine kuzibadilisha ili kuhakikisha vipimo viko sahihi kwenye eneo hilo,” alisema Kajungu. Akieleza za...

MWENYEKITI UVCCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA ATIA NIA KUGOMBEA KAHAMA

Image
Aliyekua Mwenyekiti wa Uvccm Vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Dodoma Salum Ismail amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Octoba kupiga kura katika uchaguzi mkuu.  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini amesema kuwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan ameweka mazingira rafiki kwa vijana kuweza kugombea . Amesema kuwa, aametia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kahama mjini mkoani Shinyanga. Amesema kuwa lengo la nia ya kugombea ni Kwa ajili ya kuwaketea maendeleo Wananchi wa Kibaha mjini kwani kupitia fursa nyingi zilizopo jimboni huko ikiwemo migodi ya Madini. Katika hatua nyingine Salum amekemea wanasiasa na wanaharakati wanaochochea uvunjifu wa Amani Nchini hivyo amesema kuwa watahakikisha wanapambana nao. Aidha ametoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Rais Samia kutokana na mazuri aliyoyafanya. Aidha, amesema Rais  Samia amepita katika mapito mengi lakini amehakikisha hali ya usalama wa Nchi inakuwa vizuri. "Sisi kama makanda na vijana wasomi na wa...

WADAU WA MAZINGIRA WATAKIWA KUUNGANA NA SERIKALI KUTOKOMEZA UKAN

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa rai kwa wadau wa mazingira katika ngazi zote na wananchi kwa ujumla kuungana na Serikali kwa hali na mali katika mapambano dhidi ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.  Pia, amewaomba wananchi kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kukabiliana na athari za ukame ambao unaathiri sekta mbalimbali ikiwemo maji, mifugo na kilimo ambazo zina umuhimu mkubwa kwa binadamu.  Ametoa wito huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani yaliyofanyika kitaifa leo tarehe 17 Juni, 2025 katika Manispaa ya Shinyanga. Akizungumza na viongozi na wananchi, Mhe. Khamis amesema pamoja na mambo mbalimbali Tanzania pamoja na jumuiya za kimataifa kwa kushirikisha vizazi vilivyopo na vijavyo, imejitolea kuongoa hekta bilioni moja ya ardhi iliyoharibika kufikia mwaka 2030. Alisema Tanzania ni moja ya waathir...

MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI- DKT.SAMIA

Image
  Asema baada ya Vijiji vyote Meatu kupata umeme kasi inaelekea vitongojini Ataka umeme utumike kuongeza thamani ya mazao, kilimo na ufugaji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani amesema Serikali imeendelea kupeleka maendeleo katika Wilaya ya Meatu ikiwemo ukamilishaji wa usambazaji  umeme katika Vijiji vyote 109 vya Wilaya hiyo. Dkt. Samia ameyasema hayo Juni 17, 2025 Wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu akiwa kwenye ziara ya kikazi. "Kama tulivyoahidi, hatujaishia hapo, kazi ya usambazaji umeme sasa inaendelea kwenye vitongoji lakini pamoja na jitihada hizi zote ninafahamu kuna changamoto ya umeme kutokuwa na nguvu ambayo inatatuliwa." Amesema Dkt. Samia Ameeleza kuwa, Wizara ya Nishati inatatua   changamoto hiyo  ya umeme kutokuwa na nguvu  kwa kujenga  njia ya kusafirisha umeme kutoka Shinyanga hadi Simiyu na ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme.  Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea uwepo wa umeme w...

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 107 ZAKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI SIMIYU

Image
Kapinga asema sasa Serikali inapeleka umeme kwenye Vitongoji 638 Ataja miradi ya kuimarisha umeme Simiyu Simiyu yapata mitungi ya gesi 16,275 kwa bei ya ruzuku Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetumia takribani shilingi  bilioni 107.36 kupeleka umeme kwenye Vijiji vyote  474 vya Mkoa wa Simiyu.  Kapinga ameyasema hayo leo Juni 18, 2025 wakati akitoa tathmini ya hali ya upatikanaji wa umeme Mkoa wa Simiyu na maendeleo ya usambazaji wa nishati safi ya kupikia wakati wa kuhitimisha ziara  ya kikazi ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Simiyu.  "Mheshimiwa Rais baada ya kumaliza upelekaji wa umeme kwenye Vijiji, hivi sasa tunapeleka umeme kwenye Vitongoji na hivi sasa tunatekeleza miradi ya umeme kwenye Vitongoji 638 kati ya Vitongoji 1,408 vya Mkoa wa Simiyu”. Amesema Mhe. Kapinga Ameongeza kuwa Serikali itajenga kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Simiyu kupitia mradi wa gridi imara na kuongeza kuw...