MKUTANO WA KIKANDA WA MATUMIZI BORA YA NISHATI KUFANYIKA DISEMBA 4-5, ARUSHA


Na Mwandishi wetu, Dar 

Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP, Umoja wa Ulaya (EU) na Ubalozi wa Irelaa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wameandaa mkutano wa kikanda wa matumizi bora ya Nishati utakaofanyika Desemba 4 hadi 5 jijini Arusha.

Akitoa taarifa ya mkutano huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amesema utahusisha wadau wa nishati takribani 400 wa ngazi mbalimbali ikiwemo Mawaziri, wataalam na sekta binafsi,  utajumuisha kubadilishana uzoefu na uelewa katika masuala ya nishati, fursa zilizopo na uwekezaji.


Aidha, amesema kuhusu utekelezaji wa mradi huo,Tanzania tayari imeshaandaa mkakati wa matumizi bora ya nishati wa miaka 10 (2024-2034), huku wakitoka ufadhili kwa wanafunzi wa kike katika masula ya nishati ambao wapo na ujuzi mkubwa wa kukushauri namna bora ya utumiaji nishati bora kwa gharama ndogo zaidi.

Akizungumzia pogramu ya matumizi bora ya Nishati, Mhandisi Luoga amesema ina umuhimu mkubwa nchini kwani inahusisha matumizi ya umeme kwa ufanisi na kwa ubora, inalenga kupunguza upotevu wa umeme, kupunguza gharama za umeme na kulinda mazingira.

Katika mkutano huo Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Dotto Mashaka Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, huku akitoa wito kwa  watanzania kutumia vifaa vyenye viwango vya ufanisi bora wa nishati ili kudhibiti upotevu wa umeme na kutumia gharama ndogo katika matumizi ya umeme.

Kwa upande wake, Mtaalam wa Miradi kutoka UNDP, Abbas Kitogo, amesema Mkutano huo wa kikanda, utakuwa ni sehemu ya kubadilisha ujuzi, uelewa na kuhakikisha kunakuwa na uelekeo mmoja katika matumizi bora ya nishati.

"Kwani kila mmoja akifanya juhudi za matumizi ya nishati kwa ufanisi kama wanavyoelekeza wataalam wa Nishati, tutaokoa upotevu mkubwa sana wa Nishati, tunafurahi sana kuwa sehemu yautekelezaji wa program hii ambayo imelenga kusaidia upatikanaji nishati safi kwa gharama Nafuu"


Naye, Naibu Balozi wa Ireland nchini, Mags Gaynor amesema Ubalozi huo unafurahishwa na jinsi Tanzania inavyotekeleza Programu ya Matumizi Bora ya Nishati ikiwemo kuandaa mkakati utakaopelekea Tanzania kutekeleza kwa ufanisi zaidi programu husika.

Akizungumzia Mkutano huo wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati, amesema ni hatua kubwa katika safari ya mabadiliko kuelekea kwenye matumizi bora ya nishati pamoja na kuwa njia ya kusukuma ajenda ya matumizi bora ya nishati.


Programu Meneja wa Miradi ya Nishati kutoka EU, Massimiliano Pedretti, ameipongeza Tanzania kwa utekelezaji wa programu hiyo ambayo imeonesha mafanikio makubwa na kueleza kuwa Umoja huo utaongeza muda wa utekelezaji wa programu hiyo nchini ambayo ilikuwa ikifikia ukomo mwaka huu wa 2024 lakini sasa itaisha mwaka 2025 pamoja na kutanua wigo wa kazi pamoja na ufadhili.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...