DKT. BATILDA BURIAN AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA JITAHADA ZA KUKUZA UTALII MKOANI TABORA
Na. Beatus Maganja Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kwa jitihada za dhati za kukuza utalii Mkoani Tabora. Dkt. Batilda alitoa pongezi hizo Januari 15, 2024 alipotembelewa na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda ofisi kwake akiwa katika ziara ya kikazi Kanda ya Magharibi iliyokuwa na lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na utalii zinazofanywa na TAWA Mkoani humo. Mkuu huyo wa Mkoa alisema anatambua jitihada zinazofanywa na TAWA katika kuboresha miundombinu ya utalii katika bustani ya Wanyamapori Mkoani humo ijulikanayo kama Tabora ZOO na kuishauri Mamlaka hiyo kuangalia uwezekano kuongeza miundombinu katika bustani hiyo kwa ajili ya kuongeza mapato. Vilevile, alishauri kuongeza mazao mbalimbali ya wanyamapori kama vile sumu ya nyoka ambapo alisema kuwa inahitaji utafiti zaidi. Pia Dkt. Batilda alisema ili kuendelea kuchagiza shughuli