Posts

Showing posts from September, 2024

RAIS SAMIA ANAAMINI KATIKA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI - DKT. BITEKO

Image
  📌Atoa pole kwa Familia, KKKT kifo cha Askofu Sendoro 📌Kanisa Lashauriwa Kumuenzi Askofu Sendoro kwa Vitendo 📌 Waumini Waaswa Kuishi Maisha ya Kumpendeza Mungu Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na viongozi wa dini ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao ya kitume kwa maendeleo ya Watanzania. Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 17,  2024 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mwanga, Kanisa Kuu lililopo Mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Chediel  Sendoro. Askofu Sendoro amefariki  dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Septemba 9, 2024  katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga.  “ Rais yupo tayari kushirikiana na kanisa wakati wowote ili kanisa liweze kufanya kazi zote za kitume na sisi tuk

SERIKALI YAJIPANGA KUTOKOMEZA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

Image
  Na Mwandishi wetu Dar  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria ifikapo 2030 kutokomeza maambukizi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwenye halmashauri zote nchini humo ili kuwakinga wananchi wake na magonjwa hayo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya Jenister Mhagama amesema wanatarajia hadi kufikia mwaka 2027 wawe wamevuka asilimia 95 kuelekea kutokomeza magonjwa hayo pamoja na kufanya vizuri licha ya kuwepo changamoto mbalimbali ikiwemo fedha. Amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Serikali ya uingereza imekuwa ikiisaidia wizara ya Afya, ambapo leo wamekutana na mkamwana wa mwana mfalme wa Uingereza ili kujadili magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo mabusha, matende na vikope (Trachoma) "Leo tumekutana na huyu mke wa mtoto wa mfalme ili kuonyesha maeneo ambayo tumefanya vizuri, kwani Shirika la Afya duniani linataka ifikapo mwaka  2030 tuwe tumeshapambana na magonjwa hay

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA GREEN HIPPO TRAVEL AZURU MAKUYUNI WILDLIFE PARK

Image
Astaajabishwa na wingi wa vivutio na kuahidi kuwahamasisha wageni mbalimbali kutembelea eneo hilo Mkurugenzi wa Kampuni mashuhuri  ya utalii inayofahamika kama Green Hippo Travels, Astrid Kleinveld akiwa ameambatana na rafiki yake  Naomi Rugenbrink ambao wote ni raia wa Uholanzi,   tarehe 15 septemba 2024, walitembelea eneo la Makuyuni Wildlife Park liliopo wilayani Monduli mkoani Arusha kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo na kupata fursa ya kufahamu namna wanavyoweza kufanya biashara ya utalii katika eneo hili hasa  utalii wa Kupanda Mlima na Kutembea kwa miguu. Bi Astrid na mwenzake wakiongozwa na Afisa Utalii wa eneo hilo Chacha Masase walipata fursa ya kupanda Mlima Kipara ambao unapatikana ndani ya eneo hilo wenye urefu wa mita 1900 kutoka usawa wa bahari pamoja na kufanya utalii wa Kutembea kwa miguu hivyo kufanikiwa kuona wanyamapori kwa ukaribu zaidi na kufurahia mandhari iliyopo. "Uzuri wa eneo hili ni wa kustaajabisha mnoo, tumepata uzoefu wa kipekee ambao nina imani s

KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI NLD ASISITIZA WATAFANYA KAMPENI ZA BUSARA ZA

Image
Na Ombe kilonzo Zanzibar Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Ahmed Salim Hamad, akizungumza katika kikao cha ndani na viongozi wa chama hicho kutoka Chaani, Zanzibar, alisisitiza kuwa kampeni za chama hicho zitaendeshwa kwa njia ya amani. Mhe. Ahmed aliwataka viongozi wa NLD Zanzibar kuongozwa na busara wanapoeneza sera na itikadi ya chama cha NLD,  Alisisitiza, "Chama cha NLD kitaendesha kampeni za busara, kuepuka uchochezi, udanganyifu, au vurugu, na badala yake tutaweka msisitizo kwenye hoja na sera, kwani NLD Ina sera nzuri kuliko chama chochote nchini." Aliwahimiza viongozi wa NLD kuhakikisha wanajenga mahusiano bora na wananchi wa ngazi za chini, akiwataka viongozi hao kuelewa matatizo ya wananchi na kuonyesha suluhu ya matatizo kupitia sera za chama cha NLD. "NLD haitaki kuwa kama vyama vingine vinavyolalamika bila kutoa njia za kutatua matatizo ya wananchi." Alisema Mhe. Ahmed. Chama cha NLD kipo kwenye Ziara ya

HUU HAPA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO LEO SEPT 12,2024

Image
 

KIKOSI CHA AFYA JESHI LA POLISI KIMEZINDUA KAMPENI YA KUPIMA AFYA BURE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA POLISI

Image
  KAMISHNA Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Abdallah Mpallo amesema jamii ijitokeze kupima afya  kwenye kambi zinazokuwa kimeandaliwa ili kuikomboa afya na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza. Mpallo ambaye pia anatoka kikosi cha afya alisema katika kuelekea kilele cha wiki ya Polisi shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za Afya kwa kupima magojwa mbalimbali. Mpallo alisema hayo leo Septemba 11, 2024 wakati akimuwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Afya Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Lucas Mkondya. "sisi kama kikosi cha polisi tumelenga kutoa huduma za vipimo bure kwa watu wote ili kutambua afya zao na endapo mtu atagundulika kuwa anahitaji matibabu makubwa zaidi atapewa rufaa ya kwenda hospitali kubwa ilikuendelea na matibabu zaidi. Pia tunatoa elimu kuhusu magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza hasa namna ya kijikinga na homa ya nyani (Mpox). ACP. Mpallo alisema katika kambi hiyo itatolewa elimu hukusu mguu kifundo kwani watu wengi uamini kuwa ulema

WAZIRI JAFO: WIZI WA KUCHEZEA VIPIMO NI KOSA KISHERIA

Image
 Na WMA, Mwanza Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amehimiza wananchi jijini Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kila mara wanapofanya manunuzi na kuuza bidhaa mbalimbali. Aliyasema hayo Septemba 11, 2024 wakati akifungua rasmi Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.  "Wizi wa kuchezea vipimo ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340 na hata vitabu vya dini vinakataza wizi wa vipimo," alisisitiza. Katika hatua nyingine, akizungumzia ushiriki wa Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho hayo, Afisa Vipimo Mwandamizi Mkoa wa Mwanza, Lazaro Joram alisema ni mwendelezo wa utoaji elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya vipimo kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya Mkoa wa Mwanza pamoja na nchi jirani. "WMA tunatumia Maonesho haya ili kuwawezesha wadau wetu kutambua majukumu yetu, kueleza umuhimu wa kuhakiki na kutumia vipimo sahihi na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi ya vipim

NAIBU KATIBU MKUU NLD ATOA WITO HUU KWA VIONGOZI

Image
Na Ombe Kilonzo, Zanzibar Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama cha NLD, Mhe. Khamis Said Hamad, akizungumza na viongozi mbalimbali katika ziara ya ujenzi wa chama Zanzibar, alisisitiza umuhimu wa kujipanga kwa viongozi wa NLD kuhakikisha chama kinawakomboa Watanzania Bara na Visiwani. Mhe. Khamis alibainisha kuwa NLD ina sera zinazojibu changamoto za kijamii, kiuchumi, na kisiasa, na akawataka viongozi kuzieneza sera hizo ili kuvutia wananchi zaidi. Mhe. Khasani aliongeza mwito kwa viongozi hao kuandaa wagombea wenye sifa, waaminifu, na wenye nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi kwenye ngazi za mitaa na vijiji, na hatimaye uchaguzi mkuu, hatua itakayoongeza imani ya wananchi katika chaguzi zijazo. Ziara hiyo ya siku nne, ikiongozwa na Katibu Mkuu Mhe. Doyo Hassan Doyo, inaendelea leo visiwani Zanzibar.

DOYO AFANYA ZIARA ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE NLD

Image
  Zanzibar. Katibu Mkuu wa  chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, leo tarehe 11-09-2024 amewasili Visiwani Zanzibar kwa ziara ya chama cha NLD. Katika ziara hiyo, Mhe. Doyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka upande wa Bara na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho upande wa Zanzibar, akiwemo Mwenyekiti wa chama cha NLD Taifa, Mhe. Mfaume Khamis Hassan. Mhe. Doyo na Mwenyekiti wa NLD walifanya kikao cha ndani na baadhi ya wanachama wa chama hicho upande wa Zanzibar, ambapo wote kwa pamoja walitoa mwito wa kuimarisha ujenzi wa chama na ushirikiano kati ya wanachama wa NLD kutoka Bara na Zanzibar. Akizungumza na wanachama wa NLD, Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Mfaume Khamis Hassan aliwataka wanachama wa NLD nchini kumuunga mkono Mhe. Doyo ili kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho, akimwelezea Mhe.Doyo kama mtu muadilifu na mtendaji mzuri wa kazi za chama. Mwenyekiti alisisitiza, "Hakuna chama chochote kinachoweza kumkata

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

Image
  Mahamudu Jamal na Pendo Magambo, WMA Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla ametoa wito kwa taasisi, asasi na mashirika binafsi kuimarisha ushirikiano na Wakala hiyo katika masuala yanayohusu vipimo kwa nyanja za biashara, afya, usalama na mazingira. Kihulla ametoa wito huo leo Septemba 11, 2024 alipokuwa akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini katika mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, na kufanyika jijini Dar es Salaam. Akitoa taarifa ya utendaji kazi, majukumu pamoja na mafanikio ya WMA, amesema kuwa kuna maeneo zaidi ya 17 ambayo sekta binafsi inaweza kushirikiana na WMA ili kuongeza tija katika sekta ya vipimo nchini. Ametaja baadhi ya maeneo hayo ya kivipimo kuwa ni pamoja na ukaguzi na uhakiki wa mizani, uhakiki wa mitambo ya gesi, dira za maji zilizopo kwenye matumizi, mashine za michezo ya kubahatisha, lifti za majengo na maeneo mengine. Akizungumzia Sheria inayoipa Mamlaka WMA kutekeleza majukum

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

WMA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA KWA JESHI LA POLISI ILALA

Image
 Na Mahamudu Jamal, WMA Wakala wa Vipimo (WMA) imekabidhi msaada wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Septemba 10, 2024 katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam Akiongoza makabidhiano hayo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Meneja wa Mkoa wa kivipimo Ilala Muhono Nashon alisema msaada huo ni kutokana na ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kazi baina ya WMA na Jeshi la Polisi hususani katika masuala ya jinai, ulinzi na usalama kwa maeneo mbalimbali ya ukaguzi, na nyanja nyinginezo. Meneja Muhono amebainisha kuwa ushirikiano huo baina ya WMA na Jeshi la Polisi umekuwa na tija kutokana na  Jeshi hilo kudumisha hali ya amani na usalama kwa watumishi wa WMA na wananchi kwa ujumla katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Aidha, ameongeza kuwa, WMA imekabidhi vifaa hivyo ili kuunga mkono matumizi ya TEHAMA kwa taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Jeshi la Polisi. “Vifaa hivi vita

WAKULIMA LINDI WATAKIWA KUFUATA USHAURI WA KITAALAM KWENYE KILIMO

Image
Na Mwandishi wetu  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuachana na maneno ya kusikia kutoka kwa watu wanaowaaminisha kuwa mbolea inaharibu udongo badala yake wafuate ushauri unaotolewa na wataalam wa kilimo ikiwemo kutumia mbolea kwa usahihi kwenye shughuli zao za kilimo. Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni inayotekelezwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ya Kilimo ni mbolea uliofanyika katika kijiji cha Mandawa wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi yenye lengo la kuwaelimisha wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na kuhamasisha usajili wa wakulima kwenye mfumo wa kidijitali wa mbolea za ruzuku. "Wananchi tubadilike yapo maneno yanasema ukitumia mbolea unaharibu udongo, mbolea ingekuwa inaharibu udongo mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanaolisha nchi nzima nasisi tukiwepo wasingekuwa wanazalisha mpaka sasa" Hayo maneno tunayoyaamini kutoka kwa watu wasiokuwa na utaalam, hawajaenda shule tuachane

WMA YAHIMIZA MATUMIZI YA MIZANI ILIYOHAKIKIWA KWA WAFANYABIASHARA WA GESI

Image
   Na Pendo Magambo – WMA, Dar es Salaam Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imewataka wafanyabiashara wa gesi kutumia mizani iliyohakikiwa na WMA ili kujiridhisha na usahihi wa uzito wa mitungi ya gesi kabla ya kuiuza kwa wateja. Wito huo ulitolewa Septemba 3, 2024 jijini Dar es Salaam na Afisa Vipimo Yahya Tunda kutoka WMA Mkoa wa kivipimo Ilala, wakati wa semina jumuishi iliyoandaliwa na kampuni ya Gesi ya Oryx kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote. Tunda alieleza kuwa WMA inatekeleza majukumu yake kupitia Sheria ya Vipimo sura namba 340, ambayo inasimamia matumizi ya vipimo sahihi na kwa upande wa wafanyabiashara wanaotumia mizani, sheria inawataka kutumia zile zilizohakikiwa na WMA ili kuleta usawa wa kivipimo kwenye maeneo ya biashara, afya, usalama na mazingira. “Ninawashauri wafanyabiashara pindi wanapotaka kununua mizani kufika katika ofisi zetu ili wapate ushauri wa kitaalamu kuhusu aina inayofaa kulingana na biashara wanazofanya,” alisisitiza. Aki

JESHI LA POLISI LAWANOA WAGANGA 80

Image
  Na Mwandishi wetu, Dar  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema katika kukabiliana na vitendo vya ubakaji na ulawiti Septemba,3 2024 limefanya kikao na waganga wanaojulikana kama wa tiba mbadala 80 kwa lengo la kuwaelemisha kuacha kujihusisha au kufanya ramli chonganishi. Aidha limewataka waganga hao pamoja na mambo mengine kuacha tabia ya kuwapa masharti baadhi ya wateja wao kuwa ili wafanikiwe kwenye biashara na kupata utajiri lazima wafanye vitendo viovu vya  kuwalawiti au kuwabaka watoto wadogo . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linaendelea kusimamia mikakati ya kuhakikisha usalama wa Jiji la Dar es Salaam unakuwa wa hali juu ikiwa ni pamoja na kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria  matukio ya kikatili dhidi ya watoto na wanawake yanayohusisha vitendo vya kulawiti na kubaka ambavyo wakati mwingine yanapelekea wahanga kupoteza maisha. "Katika hili

WAWEKEZAJI ZAIDI YA 10 KUSHIRIKI KONGAMANO KUBWA LA WAFANYABIASHARA

Image
  Wawekezaji zaidi ya 10 kutoka nchi mbalimbali za Afrika  wanatarajia kushiriki katika Kongamano kubwa la wafanyabiashara Afrika Mashariki “East Africa Investment Forum’ lenye lengo la kuunganisha wafanyabiashara hususani watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa umoja wa wanachana watoa huduma za kifedha kwa niia ya Teknolojia ( TAFINA), Reuben Mwatosya amesema Kongamano hilo, lililoandaliwa kwa ushirikiano na vyama vikuu vya FINTECH kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Tanzania, litafanyika Septemba 12 na 13, 2024, jijini Dar es Salaam. “Kongamano hili ni muhimu kwanza kuwaleta watu pamoja ambao wataweza kushirikiana katika sehemu mbalimbali, hivyo sasa ni wakati wa kuwaleta watu hawa pamoja kujadiliana ni vipi wataweza kufanya kazi pamoja, kujifunza ni namna gani Teknolojia hizi mfano AI zitaweza kusaidia kuon

DART NA UDART ZATAKIWA KULETA WAWEKEZAJI WAZAWA MABASI YA MWENDOKASI

Image
Na Mwandishi wetu,Dar Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa (Mb) ameutaka wakala wa mabasi yaendayo haraka (Dart) na watoa huduma za usafirishaji abiria katika jiji la Dar es Salaam na Pwani (Udart) kukaa pamoja kuleta kampuni za watanzania kuwekeza katika miradi wa mwendokasi. Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizundua mfumo wa kununulia tiketi kupitia kadi janja na mageti janja kwa akili ya mabasi yaendayo haraka ambapo amesema katika jijini hilo kuna uhaba wa mabasi yaendayo haraka 670 hivyo kutumia wawekezaji wazawa kutasaidia kuondoa kwa changamoto hiyo. "Nikiri kusema tuna changamoto ya uhaba mabasi, naagiza hadi kufikia disemba mabasi 670 yawe yamefika, bado kuna miradi inaendelea ni vyema kuwaleta wawekezaji wazawa kuja kuwekeza kwani uwezo wanao ili kumaliza changamoto ya usafiri jijini Dar es Salaam, kuliko kukaa kuwasubiri wawekezaji kutoka nje ya nchi"amesema Waziri Mchengerwa. Amesem