Posts

Showing posts from March, 2023

TAMASHA LA PASAKA LA KUMSHUKURU MUNGU KWA UONGOZI WA RAIS DKT SAMIA YAENDELEA VIZURI

Image
  Na Magrethy Katengu,HPMedia, Dar  MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama amesema maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 9, 2023 viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam yanaendelea vizuri. Msama ameyasema  hayo leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kueleza namna maandalizi ya Tamasha hilo yalipofikia na Jumla ya wanamuziki wa nyimbo za Injili waliothibitisha kushiriki. “Maandalizi ya Tamasha yako vizuri na tumejipanga vya kutosha  Tamasha hilo litakuwa ni lakipekee kwani ni urejeo mpya kwa sababu halijafanyika kwa takribani miaka saba (7) iliyopita hivyo watu wote wa dini zote mnaalikwa hakuna kiingilio ni buree"amesema Msama Msama amesisitiza kuwa  lengo la Tamasha hilo ni kuwafanya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka katika mazingira mazuri na ndiyo maana wameliweka viwanja vya Leaders Club ili iwe rahisi kila mwananchi kufika. Pia Tamasha la Pasaka litatumika kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ya uongozi

SIMBA YASEPA NA MILL 35 ZA RAIS DKT SAMIA

Image
Na Mwandishi wetu HPMedia  Klabu ya Simba nchini Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya klabu bingwa  barani Afrika baada ya kuichapa mabO 7 timu ya Hoyora Fc ya nchini Guinea.  Simba imepata ushindi huo katika mchezo wake wa hatua ya makundi uliochezwa katika uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam leo Machi 18 ambapo wanaweka historia ya kuingia kwenye nafasi hiyo kwa mara ya nne. REPORT TH Simba imefanikiwa kutinga hatua hiyo ikiwa nafasi ya pili na kujizolea pointi tisa huku Raja Casablanca ya Morocco ikiwa katika nafasi ya kwanza kwa pointi 13. Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Clatous Chama (3) dakika ya 10, 36 kwa penalti na dakika ya 70, Jean Baleke akishinda magoli mawili Dakika ya 32 na 65, huku Sadio Kanoute akishinda magoli mawili dakika ya 54 na 87. Ushindi huo wa Wekundu wa Msimbazi wanafanikiwa kujizolea milioni 35 zilizoahidiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akinunua kila bao linalofungwa kwenye michuano hiy

TMA YAELEZEA MAFANIKIO MIAKA MIWILI YA RAIS DKT SAMIA

Image
Na Mwandishi wetu,HPMedia  Imeelezwa kuwa viwango vya usahihi wa utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini –TMA kwa ujumla vimeongezeka na kufikia asilimia 88.5, ambapo katika msimu wa mvua za Vuli 2022, viwango vya usahihi vilikuwa asilimia 94.1. Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mamlaka hiyo kuhusu mafanikio ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,imesema hiyo inatokana na huduma za hali ya hewa nchini kueendelea kuboreshwa na kuimarishwa katika maeneo mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya watumiaji Kitaifa na Kimataifa. Taarifa hiyo imeeleza kuwa viwango hivyo ni juu ya kiwango cha usahihi wa utabiri kinachokubalika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) cha asilimia 70 ambapo ongezeko hilo la usahihi wa utabiri unazifanya huduma za hali ya hewa zinazotolewa nchini kuwa za uhakika na kuleta mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta zote za kiu

SERIKALI KUHAKIKISHA ULINZI NA USALAMA MAHALI PA KAZI

Image
  Na Magrethy Katengu,HPMedia, Dar  Serikali  imesema itaendelea kuheshimu mikataba ya Kimataifa kwa kuhakikisha kuwa inaweka ulinzi  na Usalama mahali pa kazi ili kusaidia  Wafanyakazi walioajiriwa au kuniajiri wanafanya kazi zao Kwa amani Ili kusaidia kuchochea Ustawi wa Jamii yenye uchumi Imara . Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kwanza ya siku Moja kuimarisha Uhusiano Bora kati ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara ,Taasisi za fedha huduma na ushauri(TUICO) na chama Cha Waajiri ATE ambapo amesema Serikali ina imani sekta zote za kazi kwani zina mchango mkubwa kuongeza Uchumi na Pato la Taifa kuongezeka . "Warsha hii ya leo itakuwa chachu na kiungo muhimu cha ushirikiano wa Waajiri,Wafanyakazi pamoja na taasisi za kifedha katika kutekeleza Maadhimio ya Shirika la kazi Duniani ILO ili kuboresha mazingira rafiki katika eneo la kazi"amesema Waziri Ha

SOMA HABARI KUBWA KATIKA MAGAZETI YA LEO MARCH 9,2023

Image
 

PITIA VICHWA VYA HABARI MBALIMBALI KATIKA MAGAZETI YA LEO MARCH 3,2023

Image
 

TMA YATOA ANGALIZO LA VIPINDI VYA MVUA KUBWA

Image

PITIA VICHWA VYA HABARI ZA MAGAZETI MBALIMBALI LEO MARCH 2,2023

Image