UWT KUNDUCHI YATOA ELIMU YA UKALITI NA MAADILI MEMA KWA WANAFUNZI 5000
Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar Umoja wa Wanawake Kata Kunduchi (UWT) imewajengea uwezo wanafunzi zaidi ya 5000kutoka Shule ya Sekondari Kondo, Shule za Msingi Pius Msekwa na Shule ya Msingi Kunduchi lengo ikiwa ni kuwataka watambue cha kufanya hasa wanapotendewa ukatili wa kijinsia ama wanapokutana nao. Akizungumza na wanafunzi katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kunduchi Twilumba Jane Balama amesema watahakikisha wanawafikia wanafunzi wote katika shule zilizopo kwenye Kata ya Kunduchi ili kuisaidia Serikali kupambana na ukatili na hasa kutengeneza kizazi kilicho bora zaidi kwa maslahi mapana ya nchi ya Tanzania. Amesema kuwa, lengo kufanya ziara hiyo ni kutokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kuongezeka siku hadi, hivyo wameona ni jambo jema kuanzia mashuleni ambako ndio kuna wahanga wakubwa. "Tumeona tuanzie mashuleni kwani watoto wengi ndio waathirika wa vitendo vya ukatili kwa hiyo tumewafikia watoto wasiopungua 5000 na kuzungumza nao kuhusu maadili mema na nam