Posts

Showing posts from August, 2024

KAMISHNA WAKULYAMBA ASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Image
  Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo  kuanzia kwen

RAIS DKT SAMIA KUHUTUBIA JUKWAA LA FOCAC, TAZARA KUFUFULIWA UPYA

Image
Na Mwandishi wetu,Dar Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa Kilele wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba 2024 jijini Beijing, China. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (MB) amesema kuwa Dkt Samia anashiriki mkutano huo kufuatia mwaliko wa  Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping. Amesema kuwa, ushiriki wa RAIS DKT Samia kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC umelenga kuendelea kudumisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China ambao mwaka huu umetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.  Pia kujadiliana na kukubaliana na Serikali ya China namna ya kuendelea kuongeza ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele kwa maendeleo ya pande ya Taifa ikiwemo katika sekta ya m

SERIKALI KUWALIPA WANAOPISHA MIRADI YA MAENDELEO

Image
Na Mwandishi wetu  Serikali imesema imekua ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanaopitiwa na miradi mbalimbali ya kimaendeleo wanalipwa stahiki zao katika maeneo yaliopitiwa na miradi ili kuhakikisha hakuna malalamiko kutoka kwa wananchi. Akizungumza na wadau mbalimbali, Kamishana wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nyanda Shuli, katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya HakiRasilimali ambapo amesema Tume hiyo imekua ikifanya kazi na wadau mbalimbali. "Tume ya haki na utawala bora imekuwa ikifanya kazi na wadau mbalimbali ikiwemo kituo cha Sheria na haki za Binadamu(LHRC) na imekuwa ikipokea malalamiko ya aina tofauti tofauti kutoka kwa wananchi nakuyaripoti Mahakamani kupatiwa utatuzi"amesema Nyanda. Aidha, katika mdahalo huo walijadili kwa kina namna sheria zinavyoweza  kumsadia mwananchi kupata haki zake pale mradi unapopita katika eneo lake ili aweze kulipwa fidia kulingana na hali halisi ya mali zilizopo "Kuna baadhi ya mikanganyiko inayoto

SERIKALI INAENDELEA NA MAJADILIANO NA KAMPUNI ZA NISHATI ZA KIMATAIFA - KAPINGA

Image
Asema majadiliano ni muhimu kwani ndio yanayoweka msingi wa kodi, mirabaha pamoja na ulinzi wa vigezo wa Nchi kunufaika kiuchumi. Asema LNG ni kipaumbele Serikalini Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali inaendelea na majadiliano na Kampuni za Nishati za Kimataifa (International Energy Companies - IEC’s) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia kuwa Kimiminika – LNG na yakikamilika Serikali itaupeleka kwenye hatua inayofuata. Mhe. Kapinga amesema hayo leo Agosti 29, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Joseph Khenani aliyetaka  kufahamu lini Serikali  itapeleka bungeni mkataba kati ya Tanzania na Wawekezaji wa Gesi asilia wenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 70 kwa ajili ya kujadiliwa. "Mradi huu unamanufaa makubwa sana kwa Taifa letu, majadiliano haya ni muhimu kwa sababu ndio yanayoweka msingi wa kodi, mirabaha pamoja na ulinzi wa vigezo wa Nchi kunufaika kiuchumi",

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

AJALI YA TRENI KIGOMA TRC YATOA TAMKO

Image
Na Mwandishi wetu, Kigoma  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa  ametembelea majeruhi wa  ajali ya treni mkoani Kigoma na kusema Serikali  itagharamia matibabu ya abiria 73 waliojeruhiwa katika ajali ya treni ya abiria iliyoanguka eneo la Lugufu wilaya ya Uvinza usiku wa kuamkia Agosti 28 mwaka huu. Kadogosa amesema  hayo  alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya rufaa ya mkoa kigoma Maweni na hospitali ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo amesema kuwa pamoja na kugharamia matibabu kwa majeruhi wote pia TRC itawasafirisha majeruhi wote wa ajali hiyo kuendelea na safari zao hadi wanapokwenda.  Akiwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk.Lameck Mdengo amesema kuwa hadi sasa wamebaki wagonjwa wanne kati ya watano waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo. Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya Uvinza, Dk.David Patrick George alisema kuwa wagonjwa 73 walipokewa hospitalini hapo siku ya ajali na hadi ku

TAMISEMI KESHO KIKAANGONI, WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA MAHAKAMA KUU DAR

Image
  Na Mwandishi wetu  Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kesho saa 8 mchana katika mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam kuskiliza hoja za mwanasheria mkuu wa Serikali kuhusu kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa vitongoji vijiji na Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mweiz Novemba mwaka 2024. Shauri hilo limefunguliwa na wananchi watatu ambao ni raia wa kitanzania dhidi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimamia uchaguzi wa mwaka huu (2024) wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji . Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii Dkt Ananilea Nkya ambaye ni miongoni wa wnanchi hao amesema kuwa maombi hayo  yatasikilizwa Jumatano wiki hii Agost, 28 Agosti 2024 katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo yatarushwa moja kwa moja  (mubashara) kupitia vyombo mbali mbali vya habari. Dkt Nkya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) amesema kuwa maombi hayo

TUGHE YATOA RAI KWA WAAJIRI KUWAPA WAFANYAKAZI HAKI YA KUJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimetoa rai kwa Waajiri nchini kuwapa wafanyakazi wao haki ya kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi ili kuleta tija katika maeneo ya kazi. Akitoa salamu za TUGHE katika ufunguzi wa Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE iliyoanza jana Jumatatu Tarehe 26 Agosti 2024, Jijini Arusha, Katibu Mkuu wa TUGHE, Cde. Hery Mkunda amesema kuwa Vyama vya Wafanyakazi ni wadau muhimu sana katika kuchangia maendeleo ya Taasisi.  Akizungumzia kuhusu Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE, Cde. Mkunda alieleza kuwa tangu mwaka 2018, TUGHE imekuwa na utaratibu wa kuandaa na kuratibu mafunzo ya pamoja yanayojumuisha washiriki toka Viongozi wa Matawi ya Chama na Mamlaka za Ajira au wawakilishi wao. “Kwa niaba ya TUGHE niwashukuru sana Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE kwa kukubali kuwezesha na kushiriki mafunzo haya ambapo tayari matunda ya uwepo wa mafunzo haya ya kila mwaka yameanza kuonekana kwani Migogoro baina ya Watumishi

TMA YAWANOA WATAALAM WA HALI YA HEWA BARANI AFRIKA

Image
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Mwakilikishi kutoka WMO (Ofisi ya Mafunzo), Bi. Eunjin CHOI akifafanua jambo katika wa mafunzo kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za Hali ya Hewa barani Afrika, Kitengo cha Elimu na Mafunzo cha Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kinachoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mwakilishi wa kudumu wa WMO, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hew ana Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a akizungumza wa mafunzo kuwajengea uwezo wataalamu wa hali ya hewa kutoka Taasisi za

DCEA YATEKETEZA EKARI 1165 ZA MASHAMBA YA BANGI

Image
  Na Mwandishi wetu, Habari Plus MAMLAKA ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama  imefanya operesheni maalum mkoani Morogoro kwa muda wa siku tisa katika vijiji vya Nyarutanga, Lujenge na Mafumbo vilivyopo wilaya za Morogoro vijijini na Kilosa.  Katika vijiji vya mafumbo na Lujenge Mamlaka imeteketeza jumla ya ekari 1,165 za mashamba ya bangi na kukamata kilogramu 102 za mbegu za bangi.  Aidha, katika operesheni iliyofanyika kijiji cha Nyarutanga  watu 6 wakiwa na kilogramu 342 za bangi wamekamatwa na watafikishwa mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika. Akizungumza mara baada ya utekelezaji wa mashamba hayo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, Mashamba ya bangi yaliyoteketezwa yamelimwa pembezoni mwa mto  Mbakana,  Misigiri na Mgeta kwenye eneo la akiba la hifadhi ya Taifa Mikumi. “Uharibifu mkubwa sana wa mazingira umefanyika katika eneo hili

OFISI YA MAKAMO WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA YAANDA MKUTANO WA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA

Image
  Na Mwandishi wetu, Dar  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imepanga kukutana na viongozi, wataalamu na wadau wa Mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kujadili changamoto za mazingira. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Ashantu Kijaji amesema kuwa mkutano huo utafanyika Septemba 09 hadi 10 , 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma ambapo mawasilisho mbali mbali yatatolewa ikiwa ni pamoja na usimamizi wa taka, nishati safi na . Amesema kuwa,  kumekuepo na changamoto mbalimbali za mazingira ambazo zinafifisha ustawi wa jamii na uchumi, ikiwa ni pamoja uharibifu wa ardhi, vyanzo ya maji, ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu. Aidha amesema kuwa Mazingira na Maliasili ni msingi wa uhai wa binadamu , hivyo usimamizi na hifadhi ya rasilimali hizo ni suala la kipaumbele na lenye umuhimu wa kipekee.  Hata hivyo, amesema kuwa cha

HUU HAPA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

TAWA YATIA SAINI MIKATABA YA UWEKEZAJI WA MIUNDOMBINU YA UTALII

Image
YATARAJIA KUIINGIZIA SERIKALI ZAIDI YA BILIONI 27 KWA MWAKA ipline, Loji zenye hadhi ya nyota 5 na Kambi za Kitalii zenye hadhi ya nyota 4 kujengwa Na. Beatus Maganja  MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA leo Agosti 24, 2024 imetia saini mikataba minne (4) ya uwekezaji wa miundombinu ya utalii na kampuni za Sea and Bush Ltd na  Ritungu Tours and Safaris Ltd Katika mapori ya Akiba ya Kijereshi, Pande na Swagaswaga na eneo la Makuyuni. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo iliyofanyika  kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis R. Semfuko amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo ni sehemu ya jitahada za TAWA katika kuunga mkono kwa vitendo maono ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza na kuendeleza biashara ya utalii nchini. Semfuko amesema kupitia uwekezaji huo, TAWA inatarajia kuingizia Serik

UWEPO WA TAWA WAONGEZA HADHI YA TAMASHA LA KIZIMKAZI - SALIM KIKEKE

Image
Na. Beatus Maganja Mtangazaji nguli, na mwandishi wa habari mashuhuri Africa Mashariki na Kati aliyekuwa akitangaza kipindi cha Dira ya Dunia katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ambaye kwasasa anafanya kazi  na Redio/TV ya Crown  FM/TV iliyopo nchini, Salim Kikeke amesema uwepo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini - TAWA katika Tamasha la Kizimkazi umekuwa chachu ya kuchagiza na kulipa hadhi tamasha hilo kutokana na Taasisi hiyo kuwapeleka wanyamapori hai ambao wamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wengi wanaotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii. Kikeke ameyasema hayo leo Agosti 21, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na kufika katika bustani ya wanyamapori hai ambapo alipata fursa ya kujionea aina mbalimbali za wanyamapori wakiwemo Simba, Chui, Fisi, Chatu, Pundamilia na spishi za aina tofauti za ndege nyuni. "Niko hapa Kizimkazi kwa ajili ya Tamasha la Kizimkazi na nimefurahi sana kutembelea banda hili la TAWA...kuna mabanda m

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI KIHENZILE ATEMBELEA BANDA LA TMA

Image
  Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile (MB) ametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kilele cha maonesho ya NaneNane 2024, Nzuguni, Dodoma.

WASANII WA BONGO MOVIE KUPEWA TUZO ZA HESHIMA ZA KIMATAIFA

Image
  Na Mwandishi wetu Wasanii wa Bongo movie wanatarajiwa kupewa heshima kimataifa kupitia Tuzo za Tamthilia zinazotarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 24,2024 Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa Kitengo cha Uhakiki kutoka Bodi ya Filamu nchini Boppe Kyungu amesema Serikali kupitia Bodi ya Filamu inazitambua tuzo hizo,ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wadau wa Filamu nchini kuungana katika kuzifanikisha kwakuwa tuzo ni nyenzo ya kuboresha Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. Aidha Kyungu ameongoza kuwa wadau wa Filamu wachangamkie Fursa hiyo kwani tuzo hizo zinaenda kuacha alama na kuona kasi mpya ya kutengeneza kazi zenye ushindani Kimataifa pamoja na kutangaza utalii na Utamaduni kupitia sekta ya Filamu nchini. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Tuzo za Tamthilia nchini Eliya Mjata amesema ujio wa tuzo hizo zinalenga kutoa fursa na wigo mpana kwa wasanii kuipa heshima tasnia na Nafasi kwa watayarishaji wa kazi za