Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar Nabii wa Taifa Dkt. Kennedy Mwasumbi kupitia huduma ya Tanzania Itubu Ministry amesema kutokana na mambo yanayoendelea kwa sasa, Tanzania hali sio nzuri, hivyo kuna haja kama taifa kufanya maombi ya kutubu. Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amekua akipata maono kuhusu nchi ya Tanzania, hivyo anaomba kuonana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwenda kumueleza kwa mustakabali wa nchi. "Nimejitokeza mbele yenu waandishinwa habari kuongea na watanzania kupitia vyombo vyenu, watanzania wanatakiwa wafanye maombi ya kutubu ili nchi iwe salama ipate utulivu, nchi yetu sio maskini lakini inahitajika kufunguliwa macho ili kuufikia utajiri uliopo,lazima tumtegemee Mungu"amesema Nabii Mwasumbi. Hata hivyo, amesema kumekuwa na mijadala mingi kupitia makundi tofauti kutumia sheria kutafsiri mambo kupitia hiyo mijadala kuna wenye hila wanaojificha nyuma ya matu...