KAWAIDA ATOA UJUMBE MZITO KWA VIJANA KUUANZA MWAKA 2025

Na Mohamed Ali Kawaida, _Mwenyekiti wa UVCCM Taifa_ Ndugu vijana wenzangu! Tukiwa tunaanza safari ya mwaka mpya wa 2025, nipende kutumia fursa hii kuwatakia heri ya mwaka mpya, afya njema, na mafanikio tele. Mwaka mpya ni fursa mpya. Ni ukurasa mwingine wa kitabu cha maisha yetu, kitabu ambacho tunaendelea kukiandika sisi wenyewe kwa bidii na maarifa yetu. Tunapokabiliana na changamoto mbalimbali, ni muhimu tukumbuke kwamba ushindi wetu haupo katika kushindana na wengine, bali katika juhudi zetu binafsi huku tukiwatakia mema wenzetu. Pia umoja na mshikamano wetu kama vijana ndiyo silaha yetu kubwa ya mafanikio. Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), nimeona kwa macho yangu nguvu, uthubutu, na bidii za vijana wa Kitanzania katika kulijenga taifa letu. Japokuwa changamoto zipo, lakini fursa ni nyingi mbele yetu, fursa ambazo tukiweza kuzitumia vizuri zitabadilisha maisha yetu na kuleta faida katika ta...