MRADI WA KUFUA UMEME WA JNHPP WAKAMILIKA RASMI: DKT BITEKO

Asema ni ndoto ya watanzania,awataka wategemee umeme wa uhakika Asisitiza kazi iliyobaki ni kuimarisha miundombinu ya kuwafikishia wananchi umeme Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Misri kuuzindua rasmi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kutegemea kupata umeme wa uhakika baada ya Mradi wa kufua umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere uliokuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa na Watanzania kukamilika rasmi. Waziri Biteko ameyasema hayo leo April 5, 2025 baada ya kutembelea Mradi huo akiwa ameambatana na Mawaziri ambao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mha. Hamadi Masauni. Amesema hivi sasa mitambo yote tisa inafanya kazi ambapo amefafanua kuwa kukamilika kwa Mradi huo kumechangiwa na maono ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan ambaye aliupokea Mradi ukiwa katika asilimia 33 ya utekelezaji wake na ndani y...